Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 10 Novemba, 2021 anatarajiwa kuondoka
nchini kuelekea Cairo nchini Misri kwa ziara ya Kiserikaliya siku tatu.
Kwa
mujibu wa taarifa ambayo imetolewa leo na Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jaffar Haniu imesema Ziara hiyo ya Kiserika li ya siku tatu inafuatia
mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.
Katika ziara hiyo,Mhe. Rais Samia pamoja
na mambo mengine anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake katika maeneo
kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo nyanja za diplomasia,
uchumi,siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii.
Mhe. Rais Samia na mwenyeji wake pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini mkataba mmoja (1) na hati saba (7) za makubalianokati ya Tanzania na Misri
Post a Comment