Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 13 Novemba, 2021 amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Adesina Akinumwi.
Katika mazungumzo hayo, Dkt. Akinumwi amempongeza Mhe. Rais Samia kwa jinsi anavyoimarisha sekta binafsi nchini Tanzania kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.
Aidha, Dkt. Akinumwi amemualika Mhe. Rais Samia kuhudhuria Jukwaa La Wawekezaji Afrika, litakalofanyika nchini Afrika Kusini mwezi Desemba ambalo litatoa fursa ya kuwakutanisha na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Dkt. Adesina Akinumwi kwa mualiko wenye lengo la kusaidia upatikanaji wa mitaji na uwekezaji wa kimkakati katika miradi ya maendeleo nchini.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwa njia ya mtandao na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank Group - AfDB) Dkt. Akinwumi A. Adesina leo tarehe 13 Novemba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment