Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* ametoa muda wa
*Miezi mitatu* kwa Shirikisho la *Vyama vya waendesha Bodaboda* Jijini humo
kuweka *Mpango kazi* kuwapanga vizuri Bodaboda ikiwa ni pamoja na utaratibu
rasmi wa *kuingia mjini na kutoka* ili kuondoa hali *uholela wa kuingia
mjini unayoendelea kwa Sasa.*
RC Makalla* ametoa
maazimio hayo wakati wa kikao Cha pamoja baina ya *Viongozi wa Bodaboda, Jeshi
la Polisi, LATRA, TARURA na TANROAD* kilicholenga kujadili *zuio la Bodaboda
kuingia mjini* lililokuwa limetolewa na Jeshi la Polisi.
Miongoni mwa
*maazimio yaliyotolewa na kikao hicho* na yanapaswa kufanyiwa kazi na
*Kamati* iliyoundwa ni pamoja na shughuli za Bodaboda kufanyika sambamba
na *kulinda taswira ya Jiji, Uwepo wa vituo rasmi vya Bodaboda
vinavyotambulika, Uvaaji wa Sare, Kofia ngumu pamoja na Bodaboda kuwa sehemu ya
kuwafichua wahalifu.*
Aidha *RC Makalla*
amesema baada ya kupatiwa *Mapendekezo ya Kamati* atahitisha kikao cha *Kamati
ya Ulinzi na Usalama* ili kuweka mazingira wezeshi ya kuhakikisha *suala la
kuingia mjini linafanyika kwa kuzingatia taratibu.*
Hata hivyo *RC
Makalla* amesema Serikali ya awamu ya sita Chini ya *Rais Samia Suluhu Hassan*
inathamini *kazi ya Bodaboda* Kutokana na shughuli hiyo *kutoa ajira kwa idadi
kubwa ya Vijana.*
Nao baadhi ya
*Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya waendesha Bodaboda* akiwemo *Said Kagomba*
ambae ndio Mwenyekiti wa Shirikisho ameishukuru Serikali kwa *kukaa meza moja*
na Shirikisho Kuangalia namna Bora ya kushughulikia Jambo hilo na wameahidi
kushirikiana na Serikali kuweka mazingira Bora ya biashara hiyo ili Bodaboda wa
Dar es salaam wawe mfano mzuri wa kuigwa.
Post a Comment