REPOA YASEMA TAFITI ZINASAIDIA KATIKA MAENDELEO YA NCHI.


Mkurugenzi wa tafiti na mafunzo kutoka Taasisi mahiri ya utafiti nchini Tanzania (REPOA ) Dkt Lucas Katera wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi katika ofisi za Taasisi hiyo.

.........................................

NA MUSSA KHALID,

Imeelezwa kuwa tafiti zinaonyesha ni vizuri kujenga mazingira ya kuwavutia wawekezaji nchini waweze kujenga ili kusaidia uzalishaji na hivyo kukuza uchumi wa nchi na kuondokana na umaskini.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na  Mkurugenzi wa tafiti na mafunzo kutoka Taasisi mahiri ya utafiti nchini Tanzania (REPOA ) Dkt Lucas Katera wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi kuhusu umuhimu na mchango wa utafiti katika maendeleo ya nchi.

Dkt Katera amesema kuwa REPOA inashughulika na ufanyaji wa tafiti mbalimbali ikiwemo kujenga uwezo na kusaidia katika utungaji wa sera katika Nyanja za ukuaji wa uchumi,pamoja na jinsia katika jamii kuhusu namna ya kunufaika na uchumi.

Amesema kuwa ni vyema utafiti ukapewa nafasi katika kutengeneza mipango ya maendeleo kwani itasaidia kuleta matokeo mazuri katika ukuaji wa nchi.

Aidha Dkt Katera amesema katika utafiti mfaidika mkubwa katika matokeo yake ni serikali pamoja na sekta binafsi kwani unasaidia kuibua changamoto mbalimbali za kusaidia kukua zaid.

Katika Hatua nyingine kuelekea miaka 60 ya Uhuru Mkurugenzi huyo wa tafiti na mafunzo REPOA amesema tafiti zimajaribu kutatua matatizo na kuweza kuyatatua yakiwemo ya huduma za jamii kama ajira,elimu na afya.

Hata hivyo ameiomba serikali  kuendelea kuonyesha mchango katika utafiti ikiwa ni pamoja na kuweka bajeti maalum ambayo itazisaidia taasisi hizo kuwa na rasilimali fedha zitakazowasaidia kufanyia tafiti zao.

0/Post a Comment/Comments