Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana la Kiinjili Tanzania Askofu Ainea Kunenha akimsimika Nae mchungaji Fredi Mtevi kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la Kiinjili.
NA SALYIM BITCHUKA
Viongozi wa Makanisa hapa nchini
wameaswa kuwa na umoja , Upendo na
Ushirikiano kwa kuwa ndio njia pekee
itakayowezesha wachungaji , Maaskofu na waumini
wao kuitangaza injili ya kweli.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki
katika Kanisa la Anglikana la Kiinjili Tanzania
Parishi ya Keko Mwanga jijini
Dar es Salaam wakati wa Ibada ya Jumapili
iliyoendana na tukio la Kusimikwa kwa
Mchungaji Fredi Mtevi .
Akizungumza mara baada ya Ibada hiyo
Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana
la Kiinjili Tanzania Askofu Ainea
Kunenha amesema kuna haja ya Viongozi
wa Makanisa kutoa elimu iliyo
sahihi ili Kanisa liweze kusonga mbele
huku akisisitiza umoja na ushirikiano katika
hilo.
Kwa upande wao baadhi ya Maskofu
waliohudhuria Ibada hiyo akiwemo Askofu
Frederick Chigwaba Kutoka Dayosisi ya
Morogoro na Mchungaji Isaya Lazaro
Chiyungu kutoka kanisa la Anglikana la Kiinjili
Tanzania Parishi ya Keko Mwanga (Mlima wa
Makimbilio ) jijini Dar es Salaam kwa
pamoja wamesema umoja na mshikamano
walionaona ndio siri kubwa ya kufanikiwa
kwa kanisa hilo huku wakisisitiza
waumini wao kupenda elimu.
Nae mchungaji Fredi Mtevi
akizungumza mara baada ya kusimikwa
Uchungaji amesema lengo la kuhamia kanisa
hilo na kusimikwa ni kwenda kutoa huduma
kwa kuwa Mungu hana mipaka huku akisisitiza
kuwa msingi mkubwa wa Kanisa ni Elimu.
‘Waumini wengi wamekuwa wakihama kutoka kanisa moja kwenda kanisa linguine
kutokana na kumtafuta Mungu wa kweli’amesema Mchungaji Fredi
Kanisa la Anglikana la Kiinjili Tanzania limepunguza madaraka ya Maaskofu huku likijikita zaidi katika kutoa huduma kwa jamii lakini bado kwa sehemu kubwa linafuata maadili ya Kanisa la Anglikana .
Post a Comment