SERIKALI KUENDELEA KUKUZA UCHUMI SHINDANI KUWEKEZA KATIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU ELIMU YA UFUNDI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wabunge wa Baraza la Wawakilishi  baada ya ufunguzi wa 25 ya utafiti ya REPOA. Novemba 10,2021.

...................................... 

NA MUSSA KHALID. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema  katika kukuza uchumi shindani serikali ya Tanzania imeendelea  kuwekeza katika kuboresha miundombinu, ukuzaji ujuzi pamoja na  elimu ya ufundi ili kuendana na mazingira shindani pamoja na ukuaji wa haraka wa teknolojia. 

Dkt Mpango amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akifungua warsha ya utafiti ya REPOA ya  25 ,warsha ilioandaliwa kwa  kushirikiano  na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Makamu wa Rais amesema katika karne ya 21 Taifa haliwezi kupata maendeleo ya haraka pasipo kutumia tafiti kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia mara kwa mara hivyo utoaji maamuzi pamoja na kupanga mipango ya maendeleo kunahitaji kuongozwa na matokeo ya tafiti.

Akizungumza na wanahabari Waziri wa Viwanda na Biashara Prof Kitila Mkumbo amesema serikali inatambua mchango wa taasisi za utafiti hapa nchini na itaendelea kupokea matokea ya tafiti hizo katika kuboresha utendaji serikalini.

Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji,maliasili na Mifugo Zanzibar DKT SOUDI Hassan ameipongeza REPOA kwa kuandaa mkutano huo kwani umesaidia katika kujadili mkakati wa kukuza uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Dkt. Donald Mmari amesema warsha hiyo ni muhimu kwa kuwa inatoa nafasi kwa watunga sera na viongozi kusikia matokeo ya tafiti pamoja na uzoefu wa nchi nyingine ili kuhuisha mipango na sera za Tanzania katika kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka zaidi. 

Naye Mwenyekiti wa Bunge na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya ViwandaBiashara na Mazingira,David Kihenzile amesema tafiti zinazofanywa na REPOA zinaisaidia serikali kuchambua mambo mbalimbali kuhusiana na uchumi wan chi. 

Warsha hiyo ya utafiti REPOA ya  25  mwaka 2021 limebeba dhima ya Mageuzi ya uchumi wa Tanzania kupitia uzalishaji viwandani na biashara shindani.

0/Post a Comment/Comments