Mwakilishi Mkazi na Mratibu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti mwenza wa Washirika wa Maendeleo Nchini Bw. Zlatan Milisic akizungumza wakati wa mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Makatibu
Wakuu kutoka wizara mbalimbali nchini na maafisa wa Serikali wakifuatilia
mawasilisho mbalimbali wakati wa mkutano wa Majadiliano ya
Kimkakati kati ya Serikali na Washirika Maendeleo uliofanyika katika Ukumbi wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mawasilisho mbalimbali katika mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba akisalimiana na Mwakilishi Mkazi na Mratibu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti mwenza wa Washirika wa Maendeleo Nchini Bw. Zlatan Milisic wakati wa mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Sauda Msemo akifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
......................................
NA SAIDINA MSANGI, DAR
ES SALAAM
Serikali imetoa wito
kwa wadau wa maendeleo kuisaidia katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa
Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2021/22-2025/26 utakao gharimu jumla ya Sh.
trilioni 114.9.
Wito huo umetolewa na
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba alipokuwa
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Majadiliano ya
Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo, jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa mkutano
huo utawezesha upatikanaji wa michango ya wadau ili kuboresha sera na miongozo
mbalimbali ili kuwezesha utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa
miaka mitano pamoja na maandalizi ya mwongozo wa uandaaji wa mipango na
bajeti ya Serikali kwa mwaka 2022/23.
“Mkutano hu utatoa
fursa kwa Wadau wa Maendeleo kuona maeneo wanayoweza kuchangia hasa katika
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano katika miradi
wanayoweza kuchangia,”alisema Bw. Tutaba.
Alitoa wito kwa wadau
wa maendeleo wanaochangia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini kutoa
ahadi zao mapema katika kuchangia bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23
ili kuiwezesha Serikali kuandaa bajeti halisi.
Alisema maandalizi ya
bajeti yatatokana na mazungumzo ya mkutano huo ambapo sekta mbalimbali
zinatarajiwa kuwasilisha zilivyojiandaa katika taasisi zao, changamoto
zilizojitokeza na mapendekezo ambayo Serikali itayaingiza kwenye bajeti.
Alisema Serikali inaendelea
kujenga mazingira wezeshi ikiwemo sera imara, kupunguza urasimu kuvutia sekta
binafsi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo
wa Taifa kwa kuchangia kiasi cha Sh. trilioni 40.6 na Serikali kuchangia kiasi
cha Sh. trilioni 74.3.
“Tunakaribisha sekta
binafsi kushiriki katika miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo utekelezaji wa
miradi iliyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa, mradi wa
ujenzi wa reli ya mwendo kasi pamoja na kuimarisha utendaji wa Shirika la Ndege
nchini-ATCL ,”alisema Bw. Tutuba.
Aidha, Bw. Tutuba
alizielekeza taasisi za elimu na utafiti nchini kufanya tafiti zitakazoiwezesha
Serikali kuboresha utoaji wa huduma na hasa maeneo yanayoweza kuibua vyanzo
vipya vya kodi ili kuchangia bajeti ya Serikali.
Mkutano huo wa siku
mbili uliohudhuriwa na makatibu wakuu, wadau wa maendeleo, asasi za kiraia,
sekta binafsi pamoja na maafisa wa serikali nchini kwa mara ya kwanza
umeshirikisha asasi za kiraia na Sekta Binafsi kutokana na mchango wake mkubwa
katika maendeleo nchini.
Kwa upande wake
Mwakilishi Mkazi na Mratibu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti mwenza wa
Washirika wa Maendeleo Nchini Bw. Zlatan Milisic ameipongeza Serikali kwa hatua
mbalimbali za kuleta mageuzi ya kijamii na kiuchumi nchini.
Bw. Milisic amepongeza
hatua ya Serikali kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuruhusiwa kurudi
shuleni kuendelea na masomo kwa mfumo wa kawaida na kuahidi kuwa wataendelea
kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya
maendeleo nchini.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa Sekta ya Binafsi Nchini Bw. Andrew Mahiga
alisema kuwa Sekta binafsi nchini iko tayari kushirikiana na Serikali
kutekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa na kuwa itachangia kuwekeza
katika sekta za kilimo, mifugo, Tehama na uchumi wa bluu kwa kuwekeza na
kushauri masuala ya sera ili kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.
Bw. Mahiga ameishukuru Serikali kwa kuijumuisha sekta binafsi katika mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya nchi na namna inavyoendelea kuishirikisha katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo na kupokea maoni yao
Post a Comment