NA MUSSA KHALID.
Serikali imeshauriwa kuonyesha muamko katika
zao la Mwani kwa kuwafundisha wataalamu wengi watakaosaidia kukiendeleza kilimo
hicho ili kukuza uchumi wan chi kupitia viwanda.
Akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa
habari hizi leo jijini Dar es salaam Mkulima wa Mwani kutoka kikundi cha
Msichoke Mlingotini Bagamoyo Mkoa wa Pwani Machano Ally Jingalao amesema
kutokana na watu kukosa uelewa wa zao hilo linaloota baharini imesababisha
kuwepo kwa changamoto ya wateja
Mzee Jingalao amesema awali walipokuwa
wakilima zao hilo walikuwa wakiwauzia matajiri kutokana na wao kuwa na mfumo
mzuri na utaratibu walikokuwa wakitumia
katika manunuzi.
‘Tulipoanza kuvuna Mwani mwaka 1995 tulikuwa
tunawauzia matajiri walikuwa wanakuja kuchukua Mwani huu kwa bahati mbaya au
nzuri wenzetu walikuwa na utaratibu mzuri sababu walikuwa wanakusaidia kamba
mpaka boto lakini wakati wakupanga bei hawatushirikishi hivyo tukaamua kuachana
nao’amesema Mzee Jingalo
Aidha Mzee Jingalao amesema ni vyema kwa
wataalamu ambao wamekwenda kusoma masuala ya Mwani wakirudi wajihusishe na
masuala ya bahari kwani imesheheni mazao mengi ambayo yanaweza kusaidia kukuza
uchumi wan chi.
Katika Hatua nyingine Mzee Jingalao amesema
changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa inaweza kusababisha Zao hilo la Mwani
kubadilika rangi na kuwa la kijana.
Hata hivyo faida ya Zao la Mwani limekuwa likitumika kwa kutengeneza Sabuni, Mafuta ya kujipaka, shampuu na vyakula vya kama Juisi,keki, jam, kachumbari na kupikwa kama mboga sambamba na utengenezaji wa dawa za Binaaadamu, vipodozi na chakula cha mifugo.
Post a Comment