Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde ameziagiza halmashauri zote katika mkoa wa songwe kukamilisha ujenzi wa madarasa kwa wakati uliotolewa na serikali ili kuruhusu wanafunzi wote waliofaulu kuanza kidato cha kwanza mwakani kutumia madarasa hayo.
Hayo ameyasema akikagua ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari mbalimbali zilipo wilaya ya Mbozi katika mkoa wa Songwe na kukuta ujenzi ukiendelea vizuri na kuagiza majengo hayo yajengwe kwa ubora na matumizi sahihi ya fedha viendane na uhalisia wa majengo hayo kama maelekezo aliyotoa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa kutoa fedha za ustawi wa Maendeleo na mapambani dhidi ya uviko 19 kujenga madarasa.
Aidha amewataka wanaosimamia ujenzi huo wamalize kwa wakati na wakitaka kumuona mbaya yasiishe kwa wakati na hatakubali shule yeyote umuangushe katika mkoa wa songwe na yeyote atayejalibu kufelisha miradi hiyo ata angaika naye mwenyewe kwa kumchukulia hatu kali za kinidhamu.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Myovizi Lenatus Stard amesema faida kubwa ya mradi huo wa ujenzi madarasa ni kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi madarasani na kero ya upungufu wa madawati hivyo kufanya wanafunzi kua na hali ya kusoma na kuongeza ufaulu zaidi.
Aidha mkuu wa shule ametaja changamoto kubwa waliyokutana nao wakati wa ujenzi ukiendelea ni kupanda kwa bei kwa baadhi ya vifaa vya ujenzi kama nondo na misumali lakini havikufanya miradi kusimama na wanauwakika wa kumaliza mwanzoni wa mwezi ujao wa december vyumba vyote vitatu.
Post a Comment