TAKWIMU ZAONYESHA NUSU YA WATANZANIA HAWAJAFIKIWA NA HUDUMA ZA KIFEDHA.


Kamishna maendeleo sekta  ya fedha kutoka wizara ya fedha na mipango Dkt Charles Mwamwaja akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea mabanda katika wiki ya maadhimisho ya kifedha kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Kamishna maendeleo sekta  ya fedha kutoka wizara ya fedha na mipango Dkt Charles Mwamwaja akizungumza wakati alipotembelea mabanda mbalimbali hapo pembeni mwa banda la  katika wiki ya maadhimisho ya kifedha kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.(picha na Mussa Khalid)

...............................

NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM 

Takwimu zimeonyesha kuwa takribani nusu ya Watanzania hawajafikiwa na huduma za kifedha nchini ambapo mpaka sasa waliofikiwa na huduma hizo ni chini ya asilimia 50 pekee. 

Hayo yameelezwa Jijini  Dar es salaam na Kamishna maendeleo sekta  ya fedha kutoka wizara ya fedha na mipango Dkt Charles Mwamwaja wakati alipotembelea mabanda katika wiki ya maadhimisho ya kifedha kitaifa ambapo amesema Elimu ya fedha ni muhimu sana Nchini. 

Amesema kuna mahusiano makubwa kati ya sekta ya fedha na maendeleo ya wananchi hivyo tayari serikali inakusudia kutoa elimu hasa kuanzia ngazi ya Elimu ya msingi pamoja na wastaafu lengo ni kutoa umuhimu wa sekta ya fedha na maendeleo ya wananchi. 

Aidha amesema kuwa ili sekta ya uchumi iweze kufanya kazi ipasavyo ni lazima kuwepo na mzungumzo mzuri wa kifedha ili kuwa na maendeleo mazuri. 

‘Tunahitaji mandeleo kwa namna yeyote ile hivyo Mabenki,Makampuni ya Bima,watu wa mitaji,watu wa Microfince wafanye kazi zao vizuri na kwa ushirikiano katika kupunguza umaskini na kutuletea maendeleo’amesema Kamishna Mwamwaja

 Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Meneja Mawasiliano wa mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania (TIRA) Elieza Rweikiza amesema wataendelea kushirikiana na serikali kutoa elimu kuhusu maswala ya bima.

Amesema uwepo wao katika maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya Bima kwani ni mtambuka hivyo wanatoa pia ushauri kwa watu wanaotaka kufungua pia biashara. 

Wiki ya maadhimisho ya huduma ya kifedha kitaifa imeanza Novemba 8 huku ufunguzi rasmi unatarajiwa kufanyika novemba 10 mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri mwenye dhamana ya fedha na mipango Dokta Mwigulu Nchemba huku wiki hiyo itahitimishwa novemba 14.

0/Post a Comment/Comments