Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
KAMPUNI ya Chocolate princess watangaza rasmi usiku wa Tamasha la vya kale dhahabu utakaofanyika disemba 10 mwaka huu Mlimani city jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi Wahabari Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mboni Masimba amesema usiku huo wa Tamasha la vya kale dhahabu ambapo ameeleza kuwa Burudani hiyo ni sehemu ya kusherehekea Miaka 60 ya uhuru wa nchi ya Tanzania.
"Tunaposherehekea Miaka 60 kila basi tunasherehekea pia Wakongwe wetu kwenye Tasnia hii ya taarab hivyo kwa mara hii tumeandaa Tamasha hili kwa ajili ya kukonga nyonyo za wapenzi wa Muziki wa mwabao hasa waimbaji taarab wakongwe".
Masimba amewataka watakao sindikiza usiku huo wa Burudani ya aina yake akiwemo Sabaha Muchacho,Khadija Kopa,Abdul Misambano,Bi.Afua Suleiman, Patricia Hillary na wengine wengi.
Hata ameongeza kuwa usiku huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwetehuku akikitaja kingilio hicho wazi kuwa ni elfu 50 za Kitanzania ikijumuishwa chakula na vinywaji.
Moja ya wadhamini katika Tamasha Hilo kutoka Kampuni ya ulinzi K4 Security Biko scanda amesema wanayofuraha kuwa sehemu ya Tamasha la vya Kale dhahabu na kuhakikisha Kuna usalama wa raia na Mali zao.
"Sisi ni sehemu ya kila historia nzuri nchini,sisi ni wakali wa Kazi zote za ulinzi na hakika tunaifanya Tanzania kujivunia Kampuni yetu."
Mkongwe wa Taarab ambae pia ni Mama mzazi wa Zuchu, Khadija Kopa amempongeza Mboni kwa kuandaa Tamasha Hilo lenye Lengo la kuwaburudisha wapenzi wa Mwambao.
"Mtoto wetu ameandaa Tamasha ambalo linatoa Burudani kwa Mashabiki zetu pia tunapata wasahaa wa kuwaenzi waliotangua kama Leila Khatib,Omary Kopa."
Meneja Masoko Kampuni ya ulinzi Ks4 Security Biko Scanda akiwatoa hofu wapenzi wa Taarab kuwa usalama utaimarika kwa kiwango Cha juu kupitia Kampuni yao katika "Tamasha la vya Kale dhahabu"
Mkongwe wa Taarab nchini Afua Suleiman akitoa pongezi kwa Muandaaji wa Tamasha Hilo Mboni Masimba kwa kuandaa Tamasha Hilo lenye Lengo la kuwapa Burudani wapenzi wa Taarab
....Mwisho....
Post a Comment