Serikali ya
Jamhuri ya Muungano imetakiwa kufikiria na
kuyakubali mapendekezo ambayo hayajakubaliwa
katika tathmini ya mapitio ya hali ya Haki
za Binadnu (UPR) kupitia mkutano 39.
Hayo
yameelezwa jana jijini Dar es Salasm na Mtandao wa
wawateyezi wa haki za binadamu ( THRDC) wakishirikiana na Kituo cha
Sheria na haki za Binadamu ( LHRC) Pamoja
na Save the Children wakati wa
wakitoa tathmini ya Ripoti ya Kikao cha
tatu cha Mapitio ya Hali ya Haki za
Binadamu ( UPR) 2021.
Akiwasilisha
ripoti hiyo Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za
Binadamu Tanzania THRDC, Bw. Onesmo Olengurumwa, amesema
Serikali inapaswa kuwashirikisha wadau
wengine wa haki za Binadamu hususan Asasi
za Kiraia na Nchi wanachama zilizotoa
mapendekezo ili kujadili uwezekano wa
kuyaboresha kulingana na mazingira halisi
ya nchi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Utetezi na Maboresho LHRC
Fulgence Masawe na Mtaalamu wa Utekelezaji
wa Haki za Watoto kutoka Save The Children
Wilbert Muchuguzi wamesema serikali
inapaswa kuangalia mapendekezo yaliyotolewa upya
hasa yale yanayogusa haki za msingi
ikiwemo haki za kiraia na Kisiasa.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa imekuwa ikishiriki katika mchakato wa Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu na mwaka huu 2021 Tanzania imefanya Mapitio ya Tatu ya UPR katika mkutano wa 39 ambapo mapendekezo 252 yalitolewa kutoka nchi mbalimbli
Post a Comment