NA MUSSA KHALID
Imeelezwa kuwa takriban migogoro zaidi ya
1000 imesuluhishwa na Ofisi ya msuluhishi wa migogoro ya Bima nchini huku kila
mwaka ikisuluhishwa migogoro zaidi ya 100 hadi 200 katika fidia na kukataliwa
kwa madai ya Bima.
Kauli hiyo imetolewa na Msajili wa Malalamiko
kutoka Ofisi Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Magreti Mngumi wakati akifanya mazungumzo na mwandishi
wa habari hizi katika maonesho ya huduma za kifedha yanayoendelea katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mngumi amesema kuwa lengo la taasisi hiyo ni
kutoa huduma za kutatua migogoro ya bima pindi mwananchi anapohitaji kudai
fidia ya bima kutokana na madhila waliyoyapata.
‘Hii ni taasisi ambayo inatoa huduma katika
utatuzi wa changamoto za wateja wa bima pale ambapo mwananchi kwa namna moja au
nyingine anapohitaji kudai fidia ya Bima mfano kwa changamoto ya amepata ajali
au chombo chake hivyo iwapo atakutana na
changamoto pindi anadai fidia ni vyema ataka kwetu ili tuweze
kumsaidia’amesema Mngumi
Aidha Msajili huyo amewataka kutumia huduma
hizo za kibima ili waweze kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili
katika maeneo yao.
Amesema ni mahali parahisi kufikika kwa
wananchi kwani migogoro mingi wanayoipokea inatokana na wahanga wa ajali
wanachopewa ni kidogo ukilinganisha na hasara waliyopata.
‘Nawajulisha wananchi kuwa ofisi hii ipo na
serikali imeianzisha kwa ajili yao na pia wiki hii tupo hapa viwanja vya mnazi
mmoja kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha kitaifa hivyo wananchi waje kwaajili ya kuwasaidia’ amesema
Mngumi
Taasisi hiyo ya serikali ya Ofisi ya Msuluhishi wa migogoro ya Bima imeanzishwa chini ya Sheria ya Bima No.10 mwaka 2009 ikiwa ni njia mbadala wa Mahakama katika utatuzi wa changamoto za wateja wa Bima.
Post a Comment