******************"*"****************
Wananchi katika mji wa Tunduma wilaya ya Momba mkoa wa Songwe wamemuomba Mbunge wao David Silinde ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwaletea gari la zimamoto ambalo litasaidia kuokoa mali wakati majanga ya moto yanapotokea tofauti na sasa wanalazimika kuomba gari la kuzimamoto kutoka nchi jirani ya Zambia au litoke makao makuu ya mkoa yaliyopo Vwawa.
Hayo yameekezwa na diwani wa kata ya Tunduma Yohana Simfukwe katika mkutano wa wafanyabiashara waliopata kuunguliwa maduka yao zaidi ya 43 siku tatu zilizopita na mbunge wa jimbo,huku akitaja sababu kubwa pia iliyochangia kutookoa mali ni ukosefu wa gari la kuzimamoto kubwa la uhakika.
Akijibu ombi hilo Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mbunge wa Tunduma David Silinde amewahaidi wananchi kumpa mda wa mwaka mmoja mpaka miwili atahakikisha gari jipya la kuzimamoto linapatikana na tayari washaweka katika mpango wa kununua mwaka ujao wa fedha kupitia mapato ya ndani ya halmashauri.
Aidha Naibu Waziri Silinde amesema wao kama halmashauri baada ya kuona waliopata majanga ya moto na kupoteza mali zao katika maduka 43 wametenga kiasi cha fedha zaidi ya milioni 200 kuwakopesha mitaji ili warudishe biashara zao za kila siku za kujiingizia kipato.
Aidha wananchi katika jimbo la Tunduma wameomba suala la ulinzi na Usalama liimalishwe zaidi kuelekea msimu wa mwisho wa mwaka kwnai sasa tabia ya uvunjaji wa nyuma na kuiba mali umeanza baadhi ya maeneo katika mji huo.
Akijibu hoja hiyo mkuu wa wilaya ya Momba Faki Lulandala amesema ulinzi utaongezwa zaidi na washawafahamu wahusika wote na wanachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya dora.
Post a Comment