Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam na Makamu Mwenyekiti wa Machinga Kariakoo Namoto Yusuph akizungumza na waandishi wa habari (picha na Mussa Khalid)
NA
MUSSA KHALID
Wafanyabiashara
wadogo maarufu kama machinga jijini Dar es salaam wameendelea kuiomba serikali
kuboresha mazingira wezeshi ya sehemu wanazopangiwa kufanya biashara zao ili waweze
kuepukana na changamoto ya kuwapata wateja.
Wakizungumza
na Mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti jijini Dar es salaam kuhusu
utekelezaji wa zoezi linaloendelea la kutakiwa kuhama na kwenda maeneo
waliyopangiwa baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema zoezi hilo linawaletea
changamoto kwa kutofahamu sehemu wanayotakiwa kwenda.
Mfanyabiashara
wa Kariakoo Ramadhani Mkata pamoja na Mama Angel wamesema ni vyema serikali
ikaendelea kuchukua jukumu la kuwapanga vyema katika maeneo waliyoyatenga ambayo
yatakuwa na changamoto ya ufanyaji wa biashara .
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam na Makamu Mwenyekiti
wa Machinga Kariakoo Namoto Yusuph amesema zoezi hilo la wamachingwa kuondoka
na kwenda walipopangwa limefanyika kwa zaidi ya asilimia 85 kwenye baadhi ya
maeneo lakini kumekuwepo na changamoto ya maeneo wanayokwenda.
‘Kwa
kusema ukweli mimi ni kiongozi ninawajibu wa kuwakilisha wengi wamachinga
wametii maeneo mengi ila changamoto kwenye maeneo ambayo wajasiriamali
wanapelekwa kutokuwa rafiki kwa ajili ya ufanyaji wa biashara’amesema Namoto
Naye
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania
Stephen Chamle baadhi ya maeneo ya soko
la Kariakoo kumekuwa na changamoto kutokubaliana na utaratibu hivyo ameiomba
serikali ya mkoa kutumia hekima kuwapeleka sehemu zitakazowasaidia kufanikiwa
na ufanyaji wa shughuli zao pasipo bugudha yeyote.
‘Sisi
kama Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania agizo la Mhe Rais tumelipokea hivyo
tunadhani ni wajibu wa mamlaka za chini kufanya utekelezaji wa jambo hili kuwa
utulivu mkubwa nikizungumzia eneo la kariakoo bado kunachangamoto ya baadhi ya
maeneo wameweza kuondoka kwa hiari lakini wengine bado wapo na ubishani usio na
afya kwa taifa kwa kutaka kuhalalisha maeneo ya barabara kufanyia biashara
’amesema Chamle
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alitoa onyo kwa wafanyabiashara wanaoendelea kufanya biashara pembezoni mwa barabara licha ya vibanda vyao kuondolewa,amewataka kuhama na kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa.
Post a Comment