Mkurugenzi wa Jukwaa la Kuwawezeshawasanii na Mpango wa bima ya Afya,kazi za sanaa (BAS) Noel Mangoma akizungumza Mara baada ya kuzindua Jukwaa Hilo na akitaja Novemba 19 kutakua na Mkutano wa kwanza wa uzinduzi wa Bima ya Afya kwa wasanii wa Sanaa zote nchini.
Muandaaji wa Mkutano kwa ajili ya kuzindua huduma ya Bima ya Afya kwa wasanii nchini Esi Mugimba akifafanua zaidi kuwa kupitia Jukwaa Hilo litaweza kuwasaidia wasanii namna ya kujitangaza kimataifa kupitia kazi za Sanaa na kuongeza kuwa Msanii jmartins kutoka Nigeria atashiriki Mkutano huo kwa njia ya Mtandao
**************************************
Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
JUKWAA la Kusaidia wasanii (BAS) wanatarajia kufungua Mkutano wa kwanza wa uzinduzi wa Bima ya Afya kwa wasanii kwa kushirikiana na wadau wa bima za Afya jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Michuzi , Mkurugenzi wa Kampuni ya Bongo sumit artist( BAS) Noel Mangoma ameeleza dhumuni la kuunda Jukwaa Hilo na kwa Mara ya kwanza kuandaa Mkutano kwa ajili ya wasanii na kutoa Elimu mbalimbali na kuhakikisha anapata wasanii wanapata bima ya Afya kwa gharama nafuu.
"Wasanii wengi nchini wanapitia changamoto ya kutomiliki kadi ya bima na ukitegemea Sanaa wanazozifanya baadhi huwaingizia pesa za kujikimuu lakini kwa upande wa bima kinakua ni kipengele kizito hivyo kuundwa kwa warsha hii itaweza kuleta Manufaa hapo mbeleni na kuwa Msaada kwao kutokana na wadau wa bima wakiwemo Mfuko wa Taifa wa bima wa Afya(NHIF) pamoja Shirika la Bima la Taifa (NIC),Jumuiya ya Hakimiliki nchini (COSOTA) kukubali kuungana nasi kutoa bima kwa wasanii"
Hata hivyo Mangoma amefafanua zaidi kuwa Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Novemba 19 mwaka huu Katika ukumbi wa library chuo cha udsm jijini Dar es salaam na kukutanisha wasanii wa fani mbalimbali ikiwemo waigizaji,Sanaa za Maonyesho,Watumbuizaji, waimbaji pamoja na Sanaa zingine ambazo zinatambulika katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
" tunategemea kuwakutanisha wasanii mbalimbali wajitokeze ili waweze kupata Elimu jinsi ya kupata bima kwa gharama nafuu na Manufaa yake,aina za bima pamoja na mengine mengi na bila kusahau Msanii kutoka Nigeria Jmartins atakuwepo kusindikiza Mkutano wetu."
Pia kwa upande wake Muandaajiwa wa Mkutano huo kutoka Kampuni ya Deal done Esi Mugimba ameongeza kuwa Msanii huyo kutoka Nigeria atashiriki Mkutano huo kupitia njia ya mtandao. " Wasanii waweze kujitokeza kwa wingi katika Mkutano huo kusikiliza na kujifunza vingi Hawa Wadau wa Afya wamewapa nafasi na wasanii kujipatia bima kwa gharama nafuu na kwa kushirikiana na wadau wasanaa waeunga Mkono asilimia zote kuanzishwa kwa Jukwaa hili kwa ajili ya kutoa Elimu shirikishi kwa wasanii namna ya kujitengeneza kikazi na kuboresha kazi zao kwa kutumia Mitandao ya kijamii.''
....Mwisho......
Post a Comment