WAVESLEEK WAJA NA SULUHISHO KWA WAPANGAJI WA NYUMBA

Mmiliki wa Kampuni ya Wavesleek Hamza Jabir akizungumza na waandishi Wahabari mara baada ya kuzindua Mtandao wa "Seto" wenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa Nyumba, sehemu za biashara Kwa wanaohitaji kupanga kupitia simu zao za Viganjani.
Baadhi ya wadau mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi wa Huduma ya kimtandao "Seto'' ya upatikanaji wa Nyumba, sehemu za biashara Kwa njia ya kiganjani.

.............................

KAMPUNI ya Wavesleek kupitia Mtandao wao wa Seto waja na suluhisho Kwa wapangaji wa nyumbani na hoteli kupitia Huduma ya kiganjani kwa bei nafuu ambapo pia inawapa fursa ya kujitengenezea kipato .

Akizungumza na waandishi Wahabari Mmiliki wa Kampuni ya Wavesleek Hamza Jabir amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto  wanaopata watu wanaotafuta Makazi pamoja na sehemu za biashara Kampuni hiyo imetambulisha rasmi Huduma ya Mtandao mpya wa "Seto" ili kusaidia upatikanaji kwa haraka na bila usumbufu wowote.

"Mtandao huu unalenga kurahisisha upatikanaji wa Nyumba, sehemu za biashara,  kupitia Mtandao wa "Setto" Kwa kupakua na kujisajiri na malipo  yake ni shilingi elfu 10 tu."

Hata hivyo ameeleza zaidi kuwa mwanzo ilikua ni usumbufu mkubwa Kwa kuwapatia Madalali pesa ya Kodi Kwa mwezi Mmoja hivyo basi kuwepo kwa Mtandao huo utaweza kusuluhisho changamoto hizo.

Jabir ameongeza kuwa Kwa vijana ambao wamekosa Ajira Kwa kupitia Huduma hiyo ya Mtandao huo "Seto" wataweza kujipatia Ajira Kwa urahisi kama Madalali.

" Nawaomba vijana wakimbilia fursa hiyo ya udalali kupitia Mtandao wa Setto Kwa kusambaza picha Kwa Nyumba ambazo zinapangishwa au kuuzwa, Kwa kufanya hivyo wataweza kupata shilingi elfu 6 kama malipo yao."

0/Post a Comment/Comments