WAZIRI WA AFYA DKT GWAJIMA AISHUKURU USAD KWA MSAADA WA T SH BILIONI 437

 



Na Richard Mrusha


Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amelishukuru shirika la misaada la watu wa marekani USAD kwa msaada wa fedha shilingi Bilioni 437 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kuboresha sekta ya afya huku serikali ya marekani ikitoa msaada wa chanjo za Janssen 165000 zilizowasili hapa nchini tarehe 13, Novemba 2021.


Pongezi hizo amezitoa jijini Dar Salaam wakati alipokutana na mtendaji mkuu wa shirika la watu wa marekani USAD V. Kate Somvongsiri aliyewasili nchini kuanza kazi rasmi baada ya yule aliyekuwepo kumaliza muda wake ambapo amewasilisha salam za serikali ya marekani kwa waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Gwajima  huku akitoa taarifa ya ujio wa chanjo zingine 500,000 aina ya Pfizer zinazotakiwa kuwasili hapa nchini Tarehe 21 Novemba 2021.


Aidha amesema kuwa serikali ya marekani imejipanga kuisaidia Tanzania kudhibiti magonjwa yanayoambukiza ikiwemo Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na Uviko 19 ambapo mwaka 2022 zaidi ya shilingi Bilioni 437 zitatolewa kutekeleza miradi ya kijamii katika kipindi cha  miaka mitano kwa lengo la kuboresha huduma sekta ya Afya na kuimarisha ustawi na maendeleo ya Vijana hapa nchini. 


Dkt Gwajima ameishukuru serikali ya Marekani kwa kuisaidia Tanzania Chanjo milioni moja zilizotolewa awali pamoja na chanjo 500,000 zinazotakiwa kuwasili hivi karibuni kwa lengo la kuongeza kasi ya uchanjaji Uviko 19 itakayo saidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa.


Aidha Dkt Gwajima amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan imejipanga kuwalinda wananchi wake kwa kudhibiti magonjwa hatarishi yanayo ambukiza hivyo ujio wa Chanjo 500,000 zitasaidia kusambazwa kwa wananchi ili wapate chanjo kwa lengo la kukabiliana na Maambukizi ya Uviko 19.


Mwisho

0/Post a Comment/Comments