Balozi wa Taulo za Kike ya "HQ" Hamisa Mobetto akikagua bidhaa hiyo mara baada ya kutangazwa nyiongeza ya ziada.
*******************************
Na.Khadija Seif, Michuzi TV
KAMPUNI ya NN General Supplies inayotengeneza taulo za kike aina ya Human Cherish ‘HQ’ kwa kuthamini elimu imetoa msaada wa Taulo za kike pakiti 92,400 kwa shule za sekondari mbalimbali hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kumthamini mtoto wakike.
Akizungumza na Michuzi Afisa Habari wa Kampuni hiyo Nosim Letara amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora bila kuwa na tatizo la kukosekana Kwa kifaa tiba .
"Tulitembelea shule mbalimbali katika Mkoa wa Dar es salaam kwa wanafunzi milioni 85 kama shukrani kwa wateja wetu, pia kuwapa taulo hili wasome vizuri bila kuwa na vikwazo vya kukosa elimu,” anasema.
Pia, Nosim ameeleza kuwa sasa bidhaa hiyo imekuja na ofa itakayodumu miaka yote ya kuongezwa Kwa pakiti 2 ambapo awali ilikua Taulo 8 na Kwa Sasa zimeongezwa zitakua 10.
“Tumeongeza pakiti mbili ofa hii itakuwa endelevu, hapo awali kuwalikuwa na taulo nane ila sasa zipo 10 kwa pakiti moja,” anasema Nosim.
Balozi wa kampuni hiyo Msanii wa muziki nchini, Hamisa Mobetto ameongeza kuwa kutokana na kuwajali wateja wa bidhaa hiyo wameona ipo haja ya kuongeza pakiti 2 Kwa Bei Ile Ile ya 3500.
Hamisa amesema kampuni hiyo imekuwa wazalendo na taifa kwa kutoa msaada wa taulo kwa shule.
“Hivi karibuni tulitoa msaada wa taulo za kike katika shule nilisoma hapo zamani, ni namna gani wanajali taifa lao na elimu kwa vijana wetu,”.
mwisho
Post a Comment