MKUMBO: WAFANYABAISHARA PUNGUZENI BEI ZA BIDHAA ILI WANANCHI WAFURAHIE SIKUKUU




Na Mwandishi wetu


WAFANYABIASHARA mbalimbali nchini, wametakiwa kupunguza bei za bidhaa na sio kupandisha katika msimu huu wa sikukuu ili kuwasaidia wananchi kupata mahitaji na kufurahia sikukuu.


Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua duka la nguo la LC Waikiki,  Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo, amesema Duniani kote kipindi cha sikukuu ni kipindi cha kufanya punguzo la bei na sio kupandisha bei.


Alisema wafanyabiashara tuachane na dhana ya kutaka kufanya bidhaa bei juu watu wakashindwa kufurahia simu kuu tuuze kwa bei elekezi wananchi wafurahie msimu wa sikukuu.


"Wakati wa sikukuu wafanyabiashara duniani kote wanafanya punguzo la bei za bidhaa na sio kupandisha, ilikuwasaidia watu kupata mahitaji."


"Niwatake wafanyabiashara wa vyakula nguo na bidhaa mbalimbali kupunguza bei ilikusaidia wananchi wafurahie msimu wa sikukuu."alisema


Pia amewapongeze wamiliki wa LC Waikiki kwa kutoa na kuongeza ajira kwa watanzania wapatao 50 na kuongeza uchumi wa nchi yetu.


"Wamesema duniani wanamaduka 1152 na hili walilolifungua sasa no duka la 1153 unaona no jinsi gani wanaweza kuwekeza na niwawekezaji wazuri katika Tanzania yetu ya viwanda." alisema Waziri Kitila Mkumbo


Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni hiyo ya LC Waikiki Micky Decha

amesema kuwa wamepanga kutoa huduma mzuri na bidhaa zenye ubora kwa wateja wao na bei nafuu.


"Tunauza bidhaa nzuri zenye ubora kwa bei nafuu tofauti na maduka mengini tupo Mlimani City upande wa chuo na ukitumia bidhaa zetu hautajuta kununua"alisema Micky Dechai

0/Post a Comment/Comments