...................
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania kupitia tawi lake la Zanzibar (THRDC-Zanzibar), na Chama cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali Visiwani Zanzibar (ANGOZA), Kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Tume ya Marekebisho ya Sheria ya Zanzibar imeandaa Mkutano wa wadau wa kupitia na kukusanya maoni kuhusu Sheria ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi visiwani Zanzibar namba 1 ya mwaka 2012.
Mkutano huo umefanyika leo Desemba 18, 2021 katika hotel ya Golden Tulip uwanja wa ndege umewahusisha wadau mbali mbali ikiwemo, Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, Tume ya Kurekebisha Sheria-Zanzibar, wanasheria mbali mbali,Pamoja na wadau wa Asasi za Kiraia visiwani humo kwa lengo la kujadili kwa kina sheria ya kuzuia rushwa na Uhujumu uchumi visiwani Zanzibar pamoja na kuangalia uwezekano wa maboresho katika maeneo kadhaa.
Pamoja na hayo washiriki wa mkutano huu wanatarajia kuangalia na kujifunza uzoefu wa nchi mbali mbali duniani katika kupambana na vitendo vya Rushwa na Uhujumu uchumi na namna Zanzibar inaweza kujifunza na kuboresha sheria hiyo kwa kutafuta mbinu mbadala, bora zaidi na zinazozingatia misingi ya haki za binadamu katika kupambana na vitendo vya Rushwa visiwani humo.
Hatua hii ni mwendelezo wa juhudi zilizoanzishwa na Mtandao wa watetetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC-Zanzibar) kwa kushirikiana na mamlaka mbali mbali katika Serikali ya mapinduzi ya Zanizibar ili kuhakikisha kunakuwa na maboresho ya sheria mbali mbali Pamoja na uzingatiwaji wa haki za binadamu katika Nyanja zote.
Post a Comment