Wakati watu mbalimbali wakiendelea na mjadala kuhusu Tanzania kukopa, Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amevunja ukimya na kueleza kuwa maendeleo makubwa hayawezi kufanyika bila kukopa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam Msama amesema kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan inapaswa kuungwa mkono na kupongezwa maana mikopo anayochukua ni kwa maslahi ya kila Mtanzania.
Amesema ni vigumu kufanya Maendeleo makubwa bila kukopa, hivyo Rais Samia Suluhu Hassan asiogopeshwe na maneno yanayozungumzwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa la Tanzania achape kazi kuilingana na anavyoona inafaa.
"Tunapohitimisha mwaka 2021 hii leo, katika mwaka 2022 tunapaswa kuwa na kauli mbiu yetu ya 'Twende na Mama Samia' hii itachochea ari ya utendaji kazi kwa Rais wetu mpendwa ambaye amefanya mambo makubwa ndani ya muda mfupi" Msama
"Zipo nchi nyingi zenye Maendeleo makubwa ambayo yametokana na mikopo yenye tija kama anayochukua Rais wetu, asitishwe achape kazi, na uwazi anaouonyesha Mhe. Rais ndiyo kitu kizuri kwa Taifa" Msama
Post a Comment