MVUA KUBWA KUNYESHA SIKU TATU DAR, PWANI, ZANZIBAR NA LINDI "TMA"




Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea kwa mvua kubwa katika maeneo ya Pwani ya Tanzania ikihusisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Visiwa vya Mafia, Lindi pamoja na Pemba na Unguja.


Tahadhari hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja wa Kituo Kikuu cha Utabiri kutoka TMA, Samwel Mbuya ambapo amesema kuwa uwezekano wa kutokea kwa mvua hiyo ni kuanzia Ijumaa ya Desemba 03, mpaka Jumatatu Desemba 06, 2021.


Aidha, athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya Makazi kuzungukwa kwa maji, ucheleweshaji wa usafiri na kusimama kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

.

 


0/Post a Comment/Comments