Isihaka Daudi ambae aliibuka Mshindi wa Michuano ya gofu katika viwanja vya lugalo jijini Dar es salaam akiongea machache mara baada ya kutangazwa Mshindi
Mshindi kutoka klabu ya lugalo Isihaka Daudi akikanyua juu kombe lake baada ya ushindi wa Mchezo wa Gofu uliodhaminiwa na Benki ya Nbc jijini Dar es salaam
**************************************
Na.Khadija Seif, Michuzi TV
MASHINDANO ya Mchezo wa Gofu yaliyoandaliwa na Benki ya Nbc kutoka klabu ya Lugalo ameibuka Mshindi kwa kupiga mikwaju 130.
Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Ally Possi amewataka viongozi wa Lugalo kuendeleza vipaji vya mchezo huo hasa Kwa watoto ili kupata wachezaji bora wa baadae
Dk. Possi alieleza kuwa watoto wakipewa msingi imara katika michezo wanafanya vizuri na kutangaza taifa kupitia vipaji vyao.
"Pongezi kwa viongozi wa klabu ya Lugalo na Chama Cha Gofu kwa kuandaa Mashindano ambayo yanaendelea vipaji vyao vijana, pia nimefurahi kusikia mshindi wa leo alianzia ngazi ya watoto hadi kucheza hatua ya watu wakubwa," alisema Possi.
Dk. Possi amewashukuru wadhamini kuwa mstari wa mbele katika kukuza michezo nchini.
Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo, Bregedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo alisema mashindano hayo mwaka huu ni mwisho katika kalenda ya Chama cha Gofu Tanzania (TGU).
Luwongo ameeleza kuwa Daudi ameipa heshima klabu ya Lugalo baada ya kushinda na kubakisha kombe nyumbani.
“Hii ni heshima kubwa ambayo ametupatia Daudi, kuhakikisha kombe hili linabaki hapa Lugalo, pia atakuja kuwa mchezaji nzuri katika siku za mbele,” alisema Luwongo.
Luwongo alisema mashindano hayo yalishirikisha klabu za Arusha, Kilimanjaro, Mufindu, Dar es Salaam Gymkhana, Zanzibar, Morogoro na mwenyeji wao Lugalo.
Mchezaji, Daudi alisema katika mashindano hayo alipata changamo nyingi kutoka kwa wachezaji wenzake ambao walikuwa chachu ya kuongeza juhudi.
"Pongezi kwa wachezaji wenzangu ambao walinipia changamoto katika mashindano, ushindi huu utakuwa chachu ya kuongeza juhudi katika mashindano mengine, " alisema Daudi.
Post a Comment