Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Shirika la Posta Tanzania linashiriki Maonesho
ya 21 ya Wajasiriamali wadogo na wa kati wa Afrika Mashariki maarufu kama
maonesho ya Nguvu Kazi /Jua Kali yanayofanyika katika viwanja vya Rock City
Mall, Jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano ya Shirika la Posta Tanzania imesema maonesho hayo yalianzishwa kwa lengo la kuwaunganisha wajasiriamali wa Afrika Mashariki ili kubadilishana ujuzi na mbinu mbalimbali za kibiashara.
Kwa mwaka huu maonesho haya yanafanyika nchini Tanzania katika
Jiji la Mwanza huyu yakibeba kauli mbiu isemayo "Kuhamasisha ubora na
uvumbuzi, ili kuongeza ushindani wa wafanyabiashara wadogo na wakati wa Afrika
Mashariki na kuinuka kiuchumi baada ya janga la uviko 19".
Posta imeshiriki maonesho haya kwa kutangaza na kutoa huduma zake mbalimbali hasa za Duka mtandao, Posta kiganjani pamoja na huduma za Usafirishaji.
Maomesho hayo yamehudhuriwa na Nchi mbalimbali za Afrika Mashariki kama vile Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, South Sudan na Tanzania mwenyewe.
Post a Comment