RAIS SAMIA KUZINDUA MRADI WA KUZALISHA VIFAA VYA UMEME KIGAMBONI

Waziri wa Viwanda (Zanzibar) mhem Omar Said Shabani akiongea na Wafanyabiashara na wawekezaji  kutoka nchini Misri na Tanzania katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC), Dkt. Maduhu Kazi akifafanua jambo katika mkutano wa wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara kutola nchini Misri mkutano uliofanyika katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam

Wafanyabiashara, wawekezaji na Viongozi mbalimbali waliofika katika mkutano huo uliofnayika katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

.......................

Wafanyabiashara zaidi ya 100 kutoka nchini misri wanatarajia kushiriki katika uzinduzi wa mradi wa kuzalisha vifaa vya umeme kutoka kampuni ya sewedy electric east Africa L.t.d.

Hayo yamejiri katika mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini misri pamoja na Tanzania lengo likiwa ni kupata taarifa za fursa za Uwekezaji zilizopo nchini.

Mkutano huo umefanyika jana Jijini Dar es salaam ambapo mara baada ya mkutano huo kituo cha uwekezaji nchini -TIC pamoja na mamlaka ya uwekezaji -GAFI wamehafikiana kuanza utekelezaji mkataba wa mashirikiano.

Aidha mkutano huo umelenga kuwakutanisha wafanyabiashara hao kutoka misri na taasisi za serikali zenye miradi ya kipaumbele ambayo inatafuta wawekezaji.

Viongozi mbalimbali wa serikali wameshiriki katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na Waziri ofisi ya waziri mkuu uwekezaji Geoffrey Mwambe, Waziri wa biashara Zanzibar Omary Said Shaaban, Naibu waziri wa nishati Steven Byabato na Mkurugenzi wa mamlaka ya uwekezaji misri Mohamed Wahab.

Uzinduzi wa mradi wa kuzalisha vifaa vya umeme kutoka kampuni ya sewedy electric east Africa L.t.d unatarajiwa kufanyika leo disemba 6 katika manispaa ya kigamboni eneo la kigogo kisarawe huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan.

0/Post a Comment/Comments