Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akionyesha mfano wa upandaji wa mti katika eneo la Mbezi Luis.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akizungumza kuelezea umuhimu wa upandaji wa Miti katika Manispaa hiyo
Mwenyekiti Mtendaji Raleigh Tanzania Society Kanda ya Pwani Caryn Khan (kushoto) wakati wa zoezi la upandaji wa miti katika eneo la Mbezi Luis Ubungo jijini Dar es salaam
Vijana wa Raleigh
Tanzania Society wakiwa pamoja na Mwenyekiti
Mtendaji wao Kanda ya Pwani Caryn Khan kwenye picha ya pamoja baada ya zoezi la
upandaji wa miti katika eneo la Mbezi Luis (picha zote na Mussa Khalid).
....................................
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Taasisi ya Raleigh Tanzania Society imepanda takriban Miti zaidi ya 2000 katika eneo la Mbezi luis Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es salaam kwa lengo la kuyatumza mazingira na kuepukana na mabadiliko ya Tabianchi.
Akizungumza wakati wa zoezi la ufanyaji wa usafi sambamba na uzinduzi wa upandaji wa Miti hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ameipongeza Taasisi hiyo kwa upandaji wa miti kwani itasaidia kuifanya Halmashuri kuwa katika Hali ya Usafi.
Mkurugenz huyo wa Ubungo ametumia fursa hiyo kuwataka wadau na Taasisi mbalimbali kuonyesha Ushirikiano kwa Manispaa hiyo katika zoezi la upandaji wa miti kwani itasaidia kuipendezesha lakini pia kukabiliana na Changamoto ya mabadiliko ya Tabia nchi.
‘Katika kufanya usafi tumeendeana na zoezi la kupanda Miti katika eneo hili lakini itaendelea kupandwa katika maeneo mengine ya Halmashauri nichukue nafasi hii kuwashukuru Raleigh International kwa kutoa Miti na kuipanda katika Manispaa’amesema Mkurugenz Beatrice
Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji Raleigh Tanzania Society Kanda ya Pwani Caryn Khan amesema katika eneo hilo wamepanda miti hiyo 2000 na zoezi hilo limekuwa ni muendelezo katika maeneo mbalimbali wakiwa na lengo la kutokomeza ukataji wa miti nchini.
Amesema kuwa katika kutekeza adhma yao ya upandaji wa miti pia wanawahamasisha watu kutumia njia mbadala pasipo kukata miti hovyo kwani kufanya hivyo ni uharibifu wa mazingira.
"Leo tupo hapa eneo la Mbezi Luis kwa kushirikiana na serikali tumeanza kufanya usafi lakini sana tumepanda miti na sisi kama Raleigh kampeni hii tunaifanya katika mikoa mitano Iringa,Dodoma Morogoro,Dar es salaam na Mwanza ni zoezi ambalo ni endelevu ambalo tunalifanya hapa nchini’amesema Caryn
Aidha Katika Kuelekea Miaka 60 ya Uhuru amewataka watanzania kuhakikisha kuwa wanapanda miti lakini pia kutumia matumizi mbadala ya nishati ili kukabiliana na mabadiliko yoyote ya kidunia.
Naye Mkuu wa Idara ya Mazingira Manispaa ya Ubungo Lawi Bernad amesema upandaji wa miti hiyo itasaidia mpaka nyakati za mvua hivyo amewaomba wadau wengine kuendelea kushirikiana ili kutengeneza mazingira ambayo wanayatumia kila siku.
Post a Comment