Na Sixmund J. Begashe
Wizara ya Maliasi
na Utalii nchini, inatarajia kuyaingiza maeneo mengi yenye sifa za kipeke na
yaliyobeba urithi adhimu wa historia, kwenye Urithi wa Dunia ili yaweze kuvuta
watalii wengi, kutoa fursa za ajira na kuchangia katika pato la Taifa.
Hayo yamesemwa na
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt Allan Kijazi alie wakilishwa na
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga kwenye ufungaji wa Mfunzo
ya namna ya kufanya maeneo yenye sifa za kipeke katika nchi za Afrika kuingia
kwenye orodha ya urithi wa Dunia.
Dkt Kijazi
awapongeza washiriki wote wa mafunzo hayo kutoka nchi mbalimbali za Afrika na
kuesema kuwa mafunzo hayo na mengine yanaendana na malengo ya kimkakati ya
Mfuko wa Urithi wa Dunia Afrika (AWHF) unaolenga kuendeleza Urithi wa Dunia kwa
Nchi Wanachama Barani Afrika.
“Mafunzo haya yamewakutanisha kwenye meza
moja wataalam, wasomi wanaosimamia Urithi wa Utamaduni na Malikale, rasilimali
hii inaujuzi na uzeofu mbukwa juu ya michakato ya Urithi wa Dunia na pia
wanauelewa mpana juu ya Mkataba unaotuongoza”. Dkt Kijazi
Kaimu Mkurugenzi
wa Malikale nchini Dkt Christowaja Ntandu, amesema Afriaka inamaeneo mengi
amabayo ni yaasili na utamaduni laini ni machache sana ambayo yapo kwenye
orodha ya Urithi wa Dunia hivyo kwa kupitia mafunzo hayo ipo nafasi kubwa kwa
wataalam kuandaa mafaili na maeneo mbalimbali yanayoweza kupendekezwa kuingia
katika urithi wa Dunia.
“Baada ya mafunzo haya wataalam wetu sasa
watakaa na kuanza mchakato wa kutambua na kuandaa maadiko ya kupendekeza maeneo
yenye sifa za kipekee ambazo zitawezesha kuingia kwenye oridha ya Urithi wa
Dunia, na Tanzania tunamaeneo mengi ambayao tunaweza kuyaingiza katika orodha
hiyo”. Dkt Ntandu
Aidha Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Urithi wa Dunia Afrika (AWHF) Bw Souyibou Varissou amesema
zipo nchi wanachama za Afrika ambazo hazina eneo hata moja kwenye orodha ya
Urithi wa Duni, hivyo amewashauri wataalam hao kutoka nchi mbalimbali za Afrika
kuungana ili kuhakikisha nchi zote zinakuwa na maeneo hayo ili kuvutia watalii
kwa wingi, kutoa ajira na uelewa mpana wa umuhimu wa maeneo hayo.
Mratibu wa Mafunzo hayo DKT James Wakiba amesema kuwa nchi takribani saba, zimeudhuria mafunzo hayo ikiwemo Tanzania, ambazo zimewasilisha maeneo yao yaweze kuchakatwa kitaalam ili kukidhi kuingizwa kwenye orodha ya Urithi wa Dunia.
Post a Comment