
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeikitoza faini ya shilingi milioni mbili kituo cha utangazaji cha wasafi Tv kwa kosa la kurusha kipindi kisicho na maadhui kwa jamii kupitia channeli yake ya youtube.
Akizunzungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Mamlaka ya Mawasiliano TCRA Hance Gunze amesema Novemba 1 mwaka huu mtangazaji wao Jordani Mwasha katika channeli ya youtube alifanya mahojiano na nabii Shilaa ambaye alitoa kauli mbaya kukejeli dini ya kikristo kwa kumuita Yesu tapeli alikua anapenda matajiri ambapo kitendo hicho ni uvunjaji wa kanuni za maaudhui
Hata hivyo amesema kutokana na kitendo hicho cha kukashifu dini ya Kikristo kituo hicho walishusha video zote na kuomba radhi kupitia kurasa zake za mtandaoni kwa watazamaji wake hivyo pamoja na kukiri na kuomba radhi TCRA wamewapa onyo kali na kuwataka kuendelea kuomba radhi kwa jamii kupitia channeli zao zote kwa kurusha tangazo litakalopigwa kila baada ya masaa manne kwa siku tatu mfululizo.
Sambamba na hayo amekitaka chombo hicho kuhakikisha shughuli zake za kuhabarisha Umma wanazingatia kanuni na sheria zilizowekwa pamoja kuajiri wafanyakazi walio na weledi na wahariri mahiri ambao kabla ya habari kurushwa wanaipitia vizuri ili kuondoa ukakasi kwa jamii na sintofahamu kwa watazamaji
“Niwaase kuhakikisha vipindi vya dini vyote viwe na wahariri mahiri wenye utaalamu waadilifu kwani kufanya hivyo kutawasadia kuepuka adhabu zisizo na tija”amesema Gunze.
Kwa upande wake mkurugenzi wa vipindit kituo cha wasafi Spensa Lameki ameishukuru Mamlaka hiyo na amekiri kutoruhusu kosa kama hilo kujirudia tena na adhabu walizopewa watazitimiza .


.
Post a Comment