………………….
Kutokana na ukosefu wa Maadili na weledi wa Utangazaji kamati ya maudhui ya mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) imekifungia kipindi cha Shule ya Uongozi
kinachotolewa kupitia Televisheni ya mtandaoni
ya Hamphrey Polepole.
Mbali na kufungiwa kwa
kipindi hicho Kamati ya Maudhui TCRA pia
imetoa onyo kali kwa televisheni hiyo ya
mtandaoni inayomilikiwa na Mbunge
wa Kuteuliwa wa CCM Hamphrey
Polepole, Uamuzi huo umetolewa
leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati
ya Maudhui ya
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Habi Gunze.
Mwenyekiti huyo
wa maudhui TCRA Habi Gunze
amesema Kituo hicho
kimekuwa kikibadili aina
ya maudhui yake
na kuwa kipindi cha
shule ya uongozi ambapo
amesema kipindi hicho kimekuwa
kikijadili masuala ya
uongozi wa kisiasa nchini pasipo kuzingatia sheria kanuni
na maadili ya uandishi
na utangazaji wa habari.
Aidha Gunze
amesema Kamati imebaini
kuwa Televisheni ya Mtandaoni Hamphrey Polepole imekuwa na mapungufu
ya kutokuwa na Wafanyakazi wenye taaluma ya waandishi na watangazaji
wa Habari jambo linalowapelekea kukiuka sheria, kanuni, msingi na maadili ya
uandishi na utangazaji wa habari katika
kazi zao kitendo
kinachopopelekea kupotosha umma na uchochezi.
Kwa upande
wake mmiliki wa Televisheni hiyo ya
Mtandaoni Mheshimiwa Hamphrey
Polepole amesema amepokea maamuzi
hayo ya kamati huku akiahidi kukaa
na wasaidizi wake na kutafakari
kwa pamoja hukumu
hiyo kisha atatoa tamko
rasmi.
Maamuzi ya hayo ni ya Shauri namba moja la mwaka 2021/2022 dhidi ya Televisheni ya mtandaoni ya Hamphrey Polepole inayomilikiwa na Mbunge wa Kuteuliwa wa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Hamphrey Polepole dhidi ya mashitaka ya ukiukwaji wa kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta ya mwaka 2020
Post a Comment