VIJANA NUNUENI NYUMBA NA SIYO KUDUNDULIZA KUJENGA :WAZIRI LUKUVI






Na Mwandishi Wetu

Vijana wametakiwa kujifunza kununua nyumba na sio kudunduliza fedha kujenga, kwa kuwa duniani kote watu hawajengi nyumba bali wananunua.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa kusherehekea miaka miwili ya jengo la Palm Village amesema Serikali na bunge limetunga sheria ina muda imetunga  sheria ya kukopa na kununua nyumba.



"Mpango wa kununua nyumba, umeanza muda mrefu, watu wanaweza kudhani Dar es Salaam imejaa lakini hawajui wanaweza kununua nyumba hata Masaki nyumba zipo zimejengwa kwa ajiri ya kuuzwa na ukinunua unapata hati yao."


"Tunasheria ya umirikishaji wa ardhi na tunasheria ya mabenki ya kukopesha fedha, kwa kuanzia serikali kupitia benki kuu kwa kuanzia imetoa zaidi ya shiringi bilioni 400 kupeleka kwenye mabenki kukopesha wananchi kwa gharama nafuu waweze kuleta maendeleo."


"Vijana ni wakati wa kununua nyumba na kumiliki hati yako, Hukiwa na mradi wa hata dora 100 ukitaka kumilikishwa ardhi utamilikishwa ili uweze kuleta maendeleo kwa watanzani."


Aidha aliongeza kuwa Kigamboni Luna viwanja zaidi ya elfu kumi ambavyo vimepangwa na kupimwa itakusaidia kutopata usumbufu wa migogoro ya ardhi.


Kwa upande wake Mkurugenzi  wa Palm Village, Jansen wa Palm,  amefuhai kwa kutimiza miaka miwili na kuwataka watu wazidi kujitokeza katika kununua na kupanga 



"Ni miaka miwili ya kulihudumia Jiji na Watu wake, miaka miwili ya kuwaweka Watu kwenye Apartments zenye ubora na usasa, miaka miwili ya kuitendea haki Mikocheni na bahari ya hindi…. Palm Village inafurahia mafanikio." amesema Jansen

0/Post a Comment/Comments