**************************************
Na Mwandishi wetu
WAANDISHI wa habari nchini Tanzania watakiwa kuandaa habari zenye utafiti kwa kutumia uandishi wao ili wananchi wafikiwe na habari zilizochakatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika mafunzo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya tafiti na kupunguza umaskini, (REPOA) Dkt Dornald Mmari amewataka waandishi kuongeza ufanisi katika kuchakata habari.
Alisema REPOA inatambia mchango na umuhimu wa waandishi wa habari na inaamini kuwa waandishi ndio wanauwezo mkubwa wa kujenga au kupomoa katika jamii.
"Waandishi wa habari tunawatengeneza ili kuweza kubadilisha fikira mbaya kwa watanzania, waandishi wanatakiwa kuandika habari zenye tafiti ili Kuweza kuwasaidia wananchi kupata habari zilizo chakatwa vizuri."alisema Dkt Mmari
Aidha alitoa mfano wa mauaji ya kimbali yaliotokea mwaka 1994 na kubainisha kwamba vyombo vya habari ndivyo vilichochea mauaji hayo.
"Mnachokiandika mnatakiwa kuwa making sana kwa kuwa mnauwezo wa kuaminisha watu na wakaamini na kuchukua nafasi kubwa juu ya mnachokiandika katika habari zenu."
Mfano mnapoanfika juu ya mradi fulani ulioshindwa kuendelea mnatakiwa kujikita na ulianzia wapi, chimbuko lake ni nini na nini kimefanya hadi umekwama, mnaweza kujikita na taasisi za utafiti ilikupata taarifa iliyoshiba zaidi."alisema Dkt Mmari
Aliongeza kuwa semina hiyo kama watafiti kunaona namna ya kuwafikia wananchi kupitia waandishi wa habari.
"Mafunzo haya tunayatoa kwa watu mbalimbali ikiwemo, Wabunge na watumishi wa umma na tutaendelea kuyatoa.
Post a Comment