Mhe
Balozi Dkt Wilbad Slaa akizungumza na Jamii ya Wairaqw waishio Dar Es Salaama
na waliotoka Mkoa wa Manyara kwenye Tamasha la kabila hilo lililofanyika Kijiji
cha Makumbusho Dar Es Salaam
Mwenyekiti wa Jamii ya Wairaqw , Dkt
Baltazary Awe akishiriki kikamilifu kwenye Tamasha hilo kwa kuburudika na
kinywaji aina Magure kwenye Tamasha la kabila hilo lililofanyika Kijiji cha
Makumbusho Dar Es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha
Makumbusho Bw Mawazo Ramadhani Jamvi akizungumza na Jamii ya Wairaqw waishio
Dar Es Salaama na waliotoka Manyara kwenye Tamasha la kabila hilo lililofanyika
Kijiji cha Makumbusho Dar Es Salaam
Mzee wa Mila wa Kabila la Wairaqw Mzee
Amatli Buxu akitoa maelekezo ya kimila kuhusu namna kinywaji cha asili ya
Kabila hilo aina ya Mangure kinavyo paswa kutayarishwa kabla ya kugaiwa kwa
watu.
Bw Reginald Malley kulia akielekezwa na mzee wa mila kutoka
Manyara namna ya kucheza bao la asili ya kabila la Wairaqw kwenye Tamasha la
kabila hilo lililofanyika Kijiji cha Makumbusho Dar Es Salaam
.............................
Jaimii
ya Wairaqw waishio Dar Es Salaam (UMBLUCHA) wamefanya tamasha kubwa Kijiji cha
Makumbusho Dar Es Salaam kwa lengo la kuhakikisha jamii ya kabila hilo
wanaoishi mijini hawaachi mila na desturi zao, kuwarithisha watoto hasa
wanaozaliwa na kuishi mijini, pamoja na kuibua mawazo ya Utalii wa mazao ya
Utamaduni.
Akizungumza na wanajumuhia ya
kabila hilo mwishoni mwa wiki Mgeni rasmi katika tamasha hilo Mhe Balozi Dkt
Willibrod Slaa amewahasa watanzania hasa wazazi kuhakikisha wanaurithisha
urithi wa utamaduni kwa kizazi kipya kwani kwa kupitia urithi huo muhimu watoto
wataendela kukua katika maadali mema.
Dkt Slaa amempongeza Mhe Rais
wa Jamuhuri ya Muungano Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele kwenye
uhifadhi wa utamaduni wa matanzania hasa kwa serikali anayoingoza kuhakikisha
imetenga hela kwa ajili ya kuboresha Kijiji cha Makumbusho kilichopo chini ya
Makumbusho ya Taifa nchini.
Akiongea kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa nchini Dkt Noel Lwoga, Kaimu Mkurugenzi
wa Kijiji cha Makumbusho Bw Mawazo Ramadhani Jamvi amesema Taasisi hiyo
imejiwekea utaratibu wa kushirikiana na Makabila mbalimbali katika kufanya
matamasha ya kiutamaduni yenye lengo la uhifadhi na urithishaji wa urithi wa
utamaduni.
Licha ya kuwapongeza Jumuia
ya Wairaq waishio Dar es Salaam kwa kuamua kuratibu tamasha hilo, Bw Jamvi
amewahakikishia kuwa Makumbusho ya Taifa itaendela kuwa karibu nao na
hata kuhakikisha ujenzi wa nyumba ya kabila hilo unafanyika kwenye Kijiji hicho
ili kuutangaza na kuhifadhi urithi wa kabila hilo.
Dkt Leonia Hambati ambaye ni
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, amesema yeye amejisikia fahari
kuendelea kudumisha utamaduni wake awapo mjini na anafanya hivyo kwa watoto
wake bila kuangalia elimu yake wala mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayo
chochoa kasi ya Utandawazi ambao unaharibu mitazamo ya vijana kuhusu utamaduni
wao.
Akiongea kwa niaba ya Jamii
ya Wairaqw (UMBLUCHA) waishio Dar es Salaam, Dkt Baltazary Awe amefafanua kuwa,
jumuhia yao imeona umuhimu wa kufanya tamasha hilo ili kujikumbushia mambo
yanayohusu Utamaduni wao, kuhakikisha watoto wao wanajifunza kutoka kwa wazee
waishio vijijini, na kuowaonesha wengine utajiri uliopo kwenye utamaduni huo.
Tamasha hilo lililochukuwa siku mbili na kufurahiwa na wageni wa ndani na nje ya nchi, lilipambwa vyema na Ngoma za asili za kabiala hilo, vyakula vya asili, majigambo, masimulizi ya wazee nyakati ya husiku, Mapishi ya Pombo maarifu ya kabila hilo ijulikanoayo kama Magure, Michezo ya Jadi, dua kutoka kwa wazee wa mila walio ombea nchi, Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na serikali ya Tanzania pamoja na Muungano nk.
Post a Comment