WANAFUNZI WATEMBEA KM 20 KUFATA ELIMU,WENGINE WAPATA MIMBA,RAIS SAMIA ATOA MILION 100 KUWASAIDIA,SILINDE KUDILI NAONWASIPO MALIZA UJENZI

 Baada ya wanafunzi katika kata ya Ikuti ambao wengi wao hukatisha masomo na wasichana wengine kupata mimba kutokana na umbali mrefu wa KM 20 kufata elimu katika shule ya sekondari ya Kyobo wilaya ya Rungwe hatimaye sasa wanaenda kutatuliwa shida hiyo baada ya kilio chao kufika kwa Rais mama Samia Suluhu.


Hayo yamebainika katika ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde kukagua fedha zilizotolewa na Rais kujenga madarasa katika wilaya hiyo na kuambiwa kiasi cha shilingi milioni mia zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitano katika kata ya Ikuti  ili kuwaepeusha wanafunzi wa kike ambao wanapata mimba ambapo kati ya wanafunzi 20 wanaonza kidato cha kwanza basi ni 12 tu ndio wanamaliza na nane wanapata ujauzito kutokana na umbali mrefu wanaotembea kufata elimu huku watoto wa kiume wakiacha masomo.


Hayo yamesemwa na katibu tawala wilaya ya Rungwe Mnkondo Bendera akieleza matumizi ya fedha za ustawi wa Maendeleo na mapambano dhidi ya uviko 19 zilizotolewa na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu kumaliza tatizo wa uhaba wa vyumba vya madarasa nchini.


Kwa upande wake Naibu Waziri David Silinde amewaagiza viongozi wa halmashauri ya Rungwe,Busekero na Kyela wakamilishe ujenzi wa madarasa hayo mapema kabla ya sikukuu ili kuruhusu wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza waanze masomo ifikapo january mwakani.


Ameongeza kuwa tarehe 31 mwezi ni siku ambayo wamepanga kumkabidhi Rais mama Samia madarasa yote 15000 yanayojengwa nchi nzima hivyo halmashauri yoyote ambayo itakwamisha ukamilishaji wa madarasa hayo watachukuliwa hatu za kinidhamu za uzembe wa kazi hivyo waharakishe mapema vya kwa viwango vizuri na thamani halisi ya fedha ionekane




0/Post a Comment/Comments