NA ISSA MOHAMED –DAR ES SALAAM.
Watanzania wametakiwa kutembelea vivutio vya ndani lengo likiwa ni
kuchochea utalii huo pamoja na kufahamu vivutio hivyo hali itakayosaidia
kutunza sehemu zenye mali kale.
Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa kampuni
ya gome safari and adventures Banzi Bryan Msumi wakati akizungumza na kituo
hiki ambapo amesema utalii wa ndani utasaidia kutunza mazingira pamoja na
kufahamu vivutio vinavyopatikana hapa nchini.
Amesema serikali imekuwa ikihamasisha uwekezaji katika sekta ya utalii
hivyo kampuni ya Gome safari and adventures inaunga mkono jitihada hizo kwa
kufanya safari za utalii huku mkakati wa mwaka 2022 kampuni hiyo imekusudia
kuongeza baadhi ya vifaa vya usafiri ikiwa ni pamoja na magari.
‘’Sisi gome safari and adventure tuna-operate katika mbuga ya saadani,
mikumi pamoja na nyerere national park pamoja na vivutio vya mali kale hasa
katika maeneo ya majumba ya wakoloni ili wakazi wa Dar es salaam waweze kufika
katika maeneo hayo, Amesema Msumi’’.
Aidha Msumi ameishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluh
Hassan katika kuhamasisha utalii huku miongoni mwa changamoto waliyokumbana na
mwaka 2020/21 ni janga la corona
Kwa upande wake tour operator wa kampuni ya gome safari and adventures,
Salehe Maulid amesema kuwa katika kutekeleza safari za utalii wamekuwa
wakizingatia utunzaji wa mazingira huku akitumia fursa hiyo kuiomba serikali
kuweka mazingira wezeshi ya miundominu.
‘’Mazingira yanajumuisha viumbe hai vyote vinavyotuzunguka hivyo
ikitokea kundi moja wapo litaharibu basi utalii nchini hautakua na tija
kutokana na hali utalii na mazingira yanashahabiana, aliongeza Saleh’’
Hata hivyo Salehe ameongeza kuwa kwa mwaka 2022 kampuni hiyo inatarajia
kuja na mpango wautalii wa kijani lengo ni kuhamasisha utunzaji wa mazingira
katika maeneo ya utalii.
Kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa –UN ya mwezi juni mwaka huu imeonesha kuwa watalii wa kimataifa wamepungua takribani bilioni 1 sawa na asilimia 73 mwaka 2020 kutokana na janga la covid-19 huku nchi zinazoendelea zimetajwa kuathirika zaidi kati ya asilimia 60 hadi 80.
Post a Comment