NA
MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Watanzania
wametakiwa kuendelea kujikinga na kuchukua tahadhari ya Mawimbi mbalimbali
yanayojitokeza ya UVIKO-19 ikiwa ni pamoja na kuchuja taarifa zinazotolewa watu
wasiokuwa na utaalamu wa magonjwa hayo.
Hayo
yameelezwa leop jijini Dar es salaam na Mtafiti Mwandamizi Taasisi ya Utafiti
wa Mgonjwa ya Binadamu (NIMRI) Dkt Kunda John Stephen wakati akifanya mahojiano
na mwandishi wa habari hizi ambapo amesema licha ya kuwepo na wagonjwa wachache wanaoripotiwa na
Wizara ya Afya nchini bado haijafikiwa hatua ya kuita wimbi la nne .
Dkt
Stephen amesema kuwa ni vyema wananchi wakasikiliza taarifa zinazotolewa na
Serikali kupitia Wizara Husika pamoja na wataalamu walioidhinishwa ili
kuepukana na changamoto katika upokeaji wa baadhi ya taarifa kuhusu maradhi
hayo.
‘Wananchi
wamekuwa wakiitegemea serikali iweze kutoa taarifa kwa kweli kumekuwa na Mawimbi
Ya Kwanza,Pili,Tatu na tumesikia kwenye baadhi ya nchi zimeripoti kuwepo na hata
hiyo OMICRON wimbi la nne lakini ingawa yote bado hayajafika Tanzania hivyo ni
vyema wananchi wakajitahidi kuchuja taarifa wanazozipata hasa wasikilize
taarifa kutoka kwa serikali’amesema Dkt Stephen
Kuhusu
suala la wananchi kuchanja chanjo ya UVIKO-19,Mtafiti huyo mwandamizi wa
NIMRI,amesema serikali imeendelea kuviimarisha vituo vya uchanjaji nchini hivyo
amewahamasisha waendelee kujitokeza kwa wingi kwani itawasaidia katika usalama
wao.
Amesema
kumekuwepo na changamoto ya watu kujisahau kujihadhari na UVIKO-19 lakini pia
taarifa potofu zinazotolewa na baadhi ya watu kuhusu ugonjwa huo hivyo
amesisitiza juhudi za ziada zinapaswa kuendelea kuchukuliwa ili mawimbi
yanayosikika katika mataifa mengine yasije yakaingia nchini.
Katika Hatua nyingine kuelekea sikukuu za mwisho wa Mwaka Krist mass na Mwaka mpya amesisitiza wananchi kuzingatia njia zote za kujikinga wasipate Uviko 19,ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka,kuvaa barakoa,pamoja na kutokushiriki sehemu zenye mikusanyiko.
Post a Comment