WIZARA YA MADINI YAKABIDHIWA TUZO YA BANDA BORA KWENYE MAONESHO ZANZIBAR




_Ni baada ya kuwa miongoni mwa mabanda yaliyotembelewa na wananchi wengi kupata huduma_

Wizara ya Madini imekabidhiwa tuzo maalum baada ya kuwa miongoni mwa mabanda bora  yaliyotembelewa na wananchi wengi kwa ajili ya kupata huduma katika maonesho ya bidhaa za viwandani yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara.

 Tuzo hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Shaaban kwenye hafla ya ufungaji wa maonesho hayo iliyohudhuriwa na viongozi wa Taasisi za Serikali pamoja na wananchi mbalimbali

Awali wakati akifunga maonesho hayo, Waziri Shaaban sambamba na kupongeza ushiriki wa Taasisi mbalimbali, amewataka washiriki kuendelea  kushiriki katika maonesho ya kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

Ameongeza kuwa serikali zote mbili zitaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza na kuzalisha ajira huku serikali zikipata mapato yak

Katika hatua nyingine, Waziri Shaaban ametembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake na kushauri ushirikiano kuendelezwa kwenye Sekta ya Madini hususan kwenye shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini.

0/Post a Comment/Comments