........................
Na.Khadija Seif, Michuzi TV
BARAZA la Sanaa la Taifa(BASATA) limetoa siku tatu Kwa wadau wa Muziki nchini kutoa maoni yao juu ya vipengele (categories) vya Tuzo za Muziki.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Matiko Mniko wakati wa Mkutano wake na waandishi Wahabari uliofanyika katika makao makuu ya ofisi zilizopo Kivukoni jijini Dar es salaam.
Aidhaa Mniko amevitaja vipengele vitakavyoshindaniwa katika Tuzo hizo na kufafanua kuwa Kuna vipengele 23 na ndani yake Kuna jumla ya Tuzo 52.
Tuzoo hizo zilizinduliwa januari 28 mwaka huu na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo ,Mhe.Mohammed Mchengerwa jijini Dar es salaam zinazotarajiwa kutolewa Marchi 26 mwaka huu baada ya washindi kupatikana kutokana na kura zitakazopigwa na wadau wa Muziki Kwa njia ya Mtandao.
Post a Comment