Mjumbe wa kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt.
Maudline Syrus Castico
...........................
Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt. Moudline Cyrus Castico Mkuu wa Idara
ya Organaizesheni ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) amesema Uhai wa Chama upo
Mashinani ikiwa ni siku ya kwanza ya Ziara ya Siku Mbili Mkoa wa Morogoro
ambapo pia ni Mlezi wa Mkoa huo Kichama
Akiwa katika ziara
hiyo ya siku Mbili Mkoa wa Morogoro kuanzia tarehe 14 - 15 Jan 2022 leo ikiwa
ni Ziara yake ya Kwanza wilaya ya Morogoro Mjini amekutana na Mabalozi wa
mashina na kufanya mikutano ya Mashina na kuwakumbusha wananchi na wanachama wa
CCM kuwa mwaka Huu 2022 kuna Matukioa makuu Mawili Moja ni Mwaka wa Uchaguzi
ndani ya Chama Cha Mapinduzi , Hivyo Watu wajitokeze kwa wingi katika kuwania
nafasi mbalimbali ndani ya Chama
Hata hivyo Katibu
wa organaizesheni Dkt. Castico amesema wanachama Waandaliwe Kisaikolojia
juu ya Uchaguzi ndani ya Chama kwa kuchagua viongozi wenye kutanguliza Mbele
Maslahi mapana ya Nchi na Chama Cha Mapindizi (CCM)
Aidha Dkt. Castico
Amesisitiza kila mtu Mwenye nia ya Kugombea ajipime na kujiuliza kwanini
anaomba nafasi ya Uongozi
“Kila mwenye nia
ya kugombea akagombee na vikao vya mapendekezo na uteuzi vikatende Haki kwa
kila Mtu bila kujali anacho au hanai“ Amesema Castico .
Dkt. Castico
amefafanua Jambo la pili Mwaka 2022 ni Sensa ya Watu na Makazi hivyo kila
Mwanachama wa CCM ni vyema akahimiza na kuelimisha jamii kuhusu Sensa
itakayofanyika ya Kuhesabu watu ili kupata idadi ya wananchi waliopo katika
ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani
Dkt. Amesisitiza
Dhamira ya Sensa 2022 ni njema kwa wananchi wa Tanzania kwa sababu
itamrahisishia Rais wetu Samia Suluhu Hassan kufikisha Maendeleo kwa wepesi
zaidi kwa kujua idadi ya watu na makazi yao kulingana na Geographia husika
“ Hata Mama
nyumbani anapika Chakula kwa kujua idadi ya wanafamilia waliopo nyumbni
“Amesema Dkt. Castico
Amemaliza kwa
kukutana na Kamati ya siasa ya wilaya ya Morogoro Mjini, Halmashauri Kuu ya CCM
wilaya ya Morogoro Mjini pamoja na Mabaraza ya Jumuiya zote Tatu , Jumuiya ya
wazazi wilaya , Jumuiya ya wanawake wilaya (UWT ) na Jumuiya ya Vijana
Wilaya (UVCCM)
Katika Kuhitimisha
Kikao hicho kizito Dkt. Amewataka viongozi wa Chama na serikali wilaya na Mkoa
waheshimu na Kuwatii Mabalozi wa Mashina na kuwatembelea pamoja na kutatua kero
za Wananchi Katika kata na Mashinani ili Kuhuisha Uhai Wa Chama Mashinani
_Huu ni Mwendelezo
wa Ziara Mashinani hadi kieleweke
Kazi iendelee
imetolewa na
IDARA YA ORGANAIZESHENI CCM TAIFA
Post a Comment