....................
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Damasa ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shindano la Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George waitara Januari 29 mwaka huu katika viwanja vya Lugalo gofu jijini Dar es salaam.
Akizungumza Afisa Habari Wa klabu ya Jeshi ya lugalo Gofu Meja Selemani Semunyu,Amesema Maandalizi yanaendelea vizuri,hali ya mvua imeendelea kuboresha viwanja kuelekea shindano hilo.
"Kwa upande wa wachezaji wameendelea kujihimarisha kuhakikisha ushindi unabaki katika klabu hiyo."
Huku zaidi ya wachezaji 100 kushiriki Shindano la "Jonnier Walker Waitara Golf Tournament 2021" litakalohusisha klabu mbalimbali ikiwemo,Dar Gymkhana,Arusha Gymkhana,Morogoro Gymkhana,Moshi,Tpc Moshi,Mufindi, na Seacleaf kutoka Zanzibar.
Post a Comment