.....................
Na.Khadija
Seif, Michuzi TV
WABUNIFU
Wa Kizanzibar wahaidi kutumia fursa ya jukwaa la Mavazi ya Kiasili kusaidia
Serikali ya Zanzibar kutangaza na kukuza pato la Taifa.
Akizungumza
na Michuzi, Mbunifu Mkongwe kutoka Visiwani Zanzibar ambae pia ni Muasisi wa
jukwaa la ubunifu (Zanzibar fashion island) Waiz Shelukindo amesema
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi julai mwaka huu likiwa
na lengo la kutangaza utalii visiwani na Mavazi ya Kiasili.
"Sanaa
ya Ubunifu wa Mavazi lazima ikue hivyo lazima kuwepo Kwa Matamasha ambayo
yanakumbusha na Kuonyesha vitu vipya hivyo tumeamua kutangaza utalii kwenye
jukwaa la ubunifu wa Mavazi linalotarajiwa kufanyika julai 29 Hadi 30 mwaka huu
katika ukumbi wa front ocean Visiwani Zanzibar."
Aidha
ameeleza kuwa jukwaa hilo litakuwa la wazi Ili kuwapa fursa watu kuhudhuria Kwa
wingi na kuona Kwa jinsi gani Kuna baadhi ya Mavazi ya Kiasili na kitamaduni
hayapewi nafasi Kwa Sasa kutokana na utandawazi na tamaduni za kizungu.
"Kuna
baadhi ya Mavazi mara nyingi yamekua hayaonekani lakini wabunifu kutokana na
kazi zao wamekuwa wakitengeneza hivyo jukwaa hilo litaweza kuwapa fursa
wabunifu kuonyesha Mavazi hayo."
Pia Waiz amesema kupitia jukwaa hilo litashirikisha wabunifu wa ndani na nje ya nchi ikiwemo Visiwa vya Comoro,Kenya, Uganda na nchi zingine nyingi Visiwani Zanzibar.
Post a Comment