KADA WA CCM MURSHID AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA HOTUBA NZURI



......,..............

KADA wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Marijani Murshid amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hotuba nzuri aliyoitoa mbele ya viongozi mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam na kidai kuwa amekuwa mfano mzuri wa kiongozi bora.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutolewa kwa hotuba hiyo na Rais Samia wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha za Uviko-19, Mushid alisema kimsingi hotuba ya Rais Samia imejaa mambo muhimu yanayolenga kuifanya Tanzania kuwa yenye maendeleo huku ikigusia suala zima la umoja.

Alisema hotuba  ya Rais Samia Suluhu Hassan imegusia masuala yote ya msingi ikiwemo faida na umuhimu wa nchi kukopa kutoka mataifa mengine, suala alilosisisitiza kuwa halina ubishi kwa kuwa linafanywa na mataifa yote duniani.

"Rais Samia alishalizungumza hili siku ile akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa Reli ya  kisasa(SGR) na baada ya hapo ni kama baadhi ya watu walitaka kumpinga hatua yake ya jana ni kama kuweka msisitizo katika hilo" alisema Murshid

Kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa madarasa, Kada huyo alisema Rais Samia hakuwa mchoyo wa fadhila baada ya kuwapongeza viongozi wote waliohusika katika usimamizi wake, jambo alilodai ni nadra kufanywa na viongozi wengine.

Aidha alisisitiza kuwa hatua ya Rais Samia pia kuwazungumzia hadharani baadhi ya viongozi walikosoa suala la nchi kukopa, kimeonyesha wazi kuwa jambo hilo halikumpendeza na zaidi lililenga kumvunja moyo katika juhudi zake za kuwaletea maendelo watanzania.

"Rais Samia amefanya vizuri kwa kitendo chake cha kuwatolea uvivu wale wote wanaompinga katika hilo, amegusia suala la uchaguzi wa Mwaka 2025, hapo naona vyema wapitishe fagio hili chama kibaki na watu safi" alisisitiza Murshid

Pamoja na hilo alisema kauli ya Rais Samia kugusia tatizo la kukatika kwa umeme akisema kuwa suala hilo halipaswi kuonekana kama anasa kwa wananchi, imelenga kuhakiksha wananchi wote wanapata huduma bora ya nishati hiyo.

0/Post a Comment/Comments