Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa kutokea Wilaya ya Temeke Mohamed Ally Mmanga alipojitokeza na kuchukua fomu ya kuwania Nafasi ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Lumumba leo jijini Dar es salaam.
Aliyewahi
kuwa Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeye
amerudisha fomu ambayo alichukua Juzi ya kuwania Nafasi ya kuteuliwa kuwa Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi ndogo za Chama Cha
Mapinduzi (CCM) zilizopo Lumumba leo
jijini Dar es salaam.
.....................................
NA
MUSSA KHALID
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu CCM Taifa kutokea Wilaya ya Temeke Mohamed Ally Mmanga amejitokeza na kuchukua fomu ya kuwania Nafasi
ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza
nimzoefu na anauwezo mkubwa katika uongozi.
Mmanga
ambaye pia aligombea Ubunge jimbo la Mbagala Dar es salaam mwaka 2020 ameeleza
hayo leo wakati akichukua fomu ya kuwania Uspika wa Bunge katika ofisi ndogo za
Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo
Lumumba jijini Dar es salaam.
Aidha
Mmanga amesema kuwa anao uwezo mkubwa yeye kama Kijana ya kuwa Spika wa Bunge
hivyo malengo yake atahakikisha anafanya kazi kwa vitendo na siyo kuwa na
maneno maneno.
‘Mimi
kama kijana ninauwezo sifa ninazo shule ipo hakuna tatizo lolote nina uwezo wa
kusimama Bungeni kusimamia mazuri ya
Bunge lakini pia kusimama na Mwenyekiti wangu wa chama Cha Mapinduzi Taifa Mama
yetu Samia Suluh Hassan hivyo mutarajie mambo mazuzi kama Chama change kitapendelea
na kunipa ridhaa hii ya kwenda kukiwakilisha bungni’amesema Mmanga
Mmanga
ameendelea kusema kwa mujibu wa Katiba inamruhusu kila raia wa Watanzania
kugombea nafasi ya Uspika hivyo atakapopata ridhaa atakwenda kufanya mazuri.
Wakati
huo huo Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Goodluck Ole Medeye amerudisha fomu ambayo alichukua Juzi ya kuwania Nafasi ya kuteuliwa
kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amesema anasubiri
vikao vya Chama viweze kuamua.
‘Namshukuru
Mungu kwa idasi ya watu waliojitokeza inaonyesha Dmokrasia katika Chama chetu
imekomaa kwamba kila mtu anafursa sawa na mwenzake kwa hivyo naupongeza Uongozi
wa Chama kwa kuweka misingi hii inayotuwezesha kushikamana’amesema Ole Medeye
Ikumbukwe mpaka sasa wamejitokeza wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya 30 ambayo wamechukua fomu ya kuwania Nafasi ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Post a Comment