PROF.NDALICHAKO AWATAKA WAAJIRI KUZINGATIA SHERIA YA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI.



Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Anayeshughulikia Kazi,ajira,vijana na wenye Ulemavu  Prof.Joyce Ndalichako akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea katika Ofisi za Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri Anayeshughulikia Kazi,ajira,vijana na wenye Ulemavu,Patrobas Katambi akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi wakati walipofanya ziara ziara ya kutembelea katika Ofisi hizo


Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi Emanuel Humba akizungumza namna ambavyo wanafanyakazi WCF.


Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Anayeshughulikia Kazi,ajira,vijana na wenye Ulemavu  Prof.Joyce Ndalichako akiwemo pia Naibu Waziri wa Wizara hiyo Patrobas Katambi kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi

.........................

NA MUSSA KHALID, 

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Anayeshughulikia Kazi,ajira,vijana na wenye Ulemavu  Prof.Joyce Ndalichako amewataka waajiri Nchini kuhakikisha wanazingatia sheria ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi ili kuweza kuwalinda pindi wanayokumbana na changamoto wawapo kazini.

Profesa Ndalichako ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kutembelea katika Ofisi za Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi ambapo amesema lengo la serikali ni kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao kwa wakati.

Aidha Profesa Ndalichako amesema ni vyema wafanyakazi wakahakikisha wanawasilisha matwakwa ya kisheria yanayohitajika kwa muda ili wawez kuhudumiwa kwa muda uliopangwa kwani mfuko huo umewekwa na serikali ili kuwasaidia watanzania. 

‘Kwa taratibu ambazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni ambazo zinasimamia mfuko huu zinatoa maelekezo mahususi ya nini mtumishi anastahili kupata kwa hiyo wafanyakazi watalipwa fidia kwa kuzingatia kile ambacho kimeanishwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za kusimamia Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi.’amesema 

Awali akizungumza Naibu Waziri Anayeshughulikia Kazi,ajira,vijana na wenye Ulemavu,Patrobas Katambi amesema ni vyema waajiri kupitia taasisi mbalimbali kujiunga na mfuko huo  huo ili waweze kuwalinda wafanyakazi wanaofanya kazi katika taasisi zao. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi Emanuel Humba amemuomba Waziri Prof .Ndalichako kuwasaidia kupata ofisi kila mkoa ili kuweza kuwa karibu na wanafanyakazi jambo litakalosaidia kuwapatia msaada wa haraka. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt John Mduma amemuhakikishia Waziri kuwa watatekeleza maagizo yote aliyowapa ikiwemo kuwa na ufanisi katika utoaji wa huduma kwani tayari wameweka misingi ya TEHAMA ili kutoa huduma zao kwa ufanisi. 

Hata hivyo Profesa Ndalicho amekipongeza kitengo cha Mipango fedha na Uwekezaji WCF kutokana na kufanya uwekezaji wenye tija na hivyo kutoa faida kwa mfuko huo.

0/Post a Comment/Comments