Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari Nape Nnauye wakati akifungua mafunzo ya utambuzi wa Anuani na Makazi
kwa wakuu wa mikoa ,wilaya pamoja na wadau mbalimbali.
................................
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Serikali imedhamiria kuwa mpaka kufika Mwezi
Mei mwaka huu kila mwananchi awe na anuani ya makazi ili kuisaidia serikali iweze
kupanga mipango yake ya maendeleo kwa urahisi.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na
Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye wakati
akifungua mafunzo ya utambuzi wa Anuani na Makazi kwa wakuu wa mikoa ,wilaya
pamoja na wadau mbalimbali.
Waziri Nape amesema kuwa anuani ya Makazi inatija kiuchumi katika
mipango mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuwezesha mtu kutoka
sehemu moja kwenda nyingine kwa haraka.
Amesema serikali itaendelea kutoa mafunzo kwa
wataalamu wa Halmashauri ili kuhakikisha kuwa utaalamu utakaopatikana uweze
utekelezaji wa mfumo katika maeneo mbalimbali nchini.
‘Mpaka sasa uwekaji wa miundombinu ya mfumo
wa Anuani za Makazi katika Mkoa wa Dar es salaam umefanyika katika Kata 46 kati ya Kata 102 ambapo jumla ya nguzo 2217 zenye mbawa za
Majina ya barabara zimesimikwa na vibawa 46,741 vya namba za Nyumba
vimebandikwa’amesema Waziri Nape
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Amos Makala amesema watahakikisha wanahamasisha suala ya Anuani ya Makazi
kuanzia ngazi za mabalozi katika mitaa jambo litakalosaidia wananchi wengi
kupata uelewa wa anuani hizo.
‘Kuwa na anuani za makazi ina faida kubwa
hivyo tunalipokea kwa furaha na kwa umoja wetu tutahakikisha elimu itawafikiwa
wana Dar es salaam wote kwa kujua faida nyingi zaidi za kujua umuhimu wa Anuani
za Makazi katika mkoa huu na Tanzania kwa ujumla’amesma RC Makala
Naye Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo amesema wameamua kuanzisha huduma hiyo Anuani ya Makazi kwa lengo la kusaidia kurahisisha huduma kwa wananchi ikiwemo huduma ya Posta Mtandao Mlangoni.
Post a Comment