TAKUKURU TEMEKE YAWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA VITENDO VYA RUSHWA.


Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Temeke  Christopher Myava akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam (hawapo pichani)

...........................

NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Temeke  jijini Dar es salaam imewaomba viongozi wa dini katika nyumba zao za ibada kutumia nafasi ya mahubiri kukemea vitendo vya Rushwa ili jamii iweze kukidhi katika maadili yasiyokuwa na Rushwa.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa TAKUKURU (M) Temeke Christopher Myava wakati akizungumza na wanahabari akitoa taarifa ya kipindi cha miezi mitatu kuanzi mwezi Octoba mosi mpaka 31/12 mwaka jana.

Myava amesema kuwa katika kipindi hicho wameweza kupokea jumla ya malalamiko mia moja na hamsini na tano ambapo kati ya hayo malalamiko 96 yamehusu Rushwa na 59 yalikuwa hayahusiani na rushwa .

Myava amesema wameanza uchunguzi wa malalamiko 96 yanayohusu rushwa, huku majalada 7 uchunguzi wake ukiwa umekamilika, 11 yamefungwa kwa kukosa ushahidi na 78 uchunguzi wake unaendelea. 

‘Jumla ya mashauri 22 yanaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Temeke’amesema Myava

Aidha Mkuu huyo wa TAKUKURU Temeke amevitaja vipaumbele katika kipindi cha Januari –Machi mwaka huu ambapo amesema watahakikisha wanaongeza kasi ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kuziba mianya hasa katika ujenzi wa miradi ya maendeleo  ambayo serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi.

Amesema kuwa TAKUKURU Mkoa wa Temeke wanaendelea kutoa elimiu kupitia Makundi mbalimbali yenye kuhamasisha wananchi ili kuongeza uelewa katika mapambano dhidi ya rushwa. 

Katika hatua nyingine Myava amewaomba viongozi wa dini kuendelea kukemea vitendo vya Rushwa katika nyumba zao za ibada kwani kutoa au kupoka Rushwa imekemewa hata katika vitabu vitakatifu.

Hata hivyo Mkuu huyo wa TAKUKURU amewakumbusha wananchi kuwa ni vyema wakatanguliza mbele maslahi ya nchi na kuchukua hatua madhubuti katika kukabiliana na tatizo la Rushwa katika mkoa huo kwani ni adui wa haki na inaweza kuathiri mgawanyo wa rasilimali katika jamii.

0/Post a Comment/Comments