***************
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Tanzania (THRDC), leo umetembelewa na Shirika Mwanachama wa mtandao
linalojishughulisha na utetezi wa Haki za vijana na makundi maalum TAYOBECO kwa
lengo la kuimarisha shughuli za utetezi wa haki za vijana na makundi maalum kwa
mwaka wa 2022 .
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa
na Afisa Habari, THRDC imesema katika kikao hicho Mkurugenzi wa TAYOBECO,Bi.
Shida Kabulunge akiambatana na maafisa wengine wanne (4) wa TAYOBECO akiwemo
Mwakilishi wa vijana NacoNGO Bw. Rogers Fungo kwa pamoja wamepata fursa
ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mratibu kitaifa wa mtandao, Bw.
Onesmo Olengurumwa pamoja na Afisa dawati la wanachama Bi. Lisa Kagaruki.
TAYOBECO wamejadiliana juu ya namna
bora ya kuimarisha mashirikiano baina yake na THRDC kama wanachama wa mtandao,
na namna wanaweza kutumia fursa zilizopo katika mtandao huo.
Moja ya eneo kubwa ambalo TAYOBECO
imehitaji kushirikiana na Mtandao ni katika upatikanaji msaada wa kisheria,
elimu ya usalama wa kidigitali pamoja na namna ya kupata fursa za kukutana na
wadau watakaiwezesha taasisi katika upatikanaji wa rasilimali fedha.
Mazungumzo hayo ni mwendelezo wa
mazungumzo yaliyofanyika mwaka jana (2021) baina ya mtandao na taasisi hii ya
TAYOBECO uliolenga kuendeleza mashirikiano baina ya taasisi hizi mbili, lakini
pia THRDC imekuwa ikiwaunganisha wanachama wake na fursa mbali mbali
zinazopatikana kutoka kwa wadau kwa lengo la kuimarisha na kukuza shughuli za
utetezi wa haki za binadamu nchini.
Post a Comment