Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kikao cha wadau wanaohusika na usafirishaji wa Kemikali hatarishi leo jijini Dar es salaam.
Albert Swai kutoka kampuni ya CMTL Logistic ambao
wanahusika na usafirishaji wa kemikali akiwaeleza waandishi wa habari namna wanavyofanya
shughuli zao za usafirishaji wa kemikali.
...............................
NA MUSSA KHALID
Wasafirishaji wa Kemikali nchini Tanzania
wametakiwa kufata muongozo wa usafirishaji kutoka kwa Mkemia Mkuu kuhusu kuwa
na vifaa vya kujikingia ili waweze kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza
wawapo safarini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam
na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt Fidelice Mafumiko wakati akifungua kikao cha
wadau wanaohusika na usafirishaji wa Kemikali hatarishi wakiwemo wawakilishi wa
serikali TRA,LATRA,Mamlaka ya Bandari Pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti na
Kupambana na Rushwa.
Dkt Mafumiko amesema kuwa malengo
yao ni kuhakikisha wanawakumbushana wasafirishaji hao sheria inayohusika
na udhibiti wa kemikali zikiwemo hatarishi pamoja na kanuni zake.
‘Lengo kuu la udhibiti au usimamizi wa kemikali
hizi hatarishi ni kulinda Afya ya wananchi pamoja na mazingira ya viumbe wote
hai unakuta kwamba uingizaji wa kemikali hizi kwa sasa hivi imeanza kuja kwa
wingi hivyo tunachofanya ni kuwafundisha wasafirishaji ili wafahamu nini
wanapaswa kukifanya wanapokuwa wanasafirisha kmikali hatarishi’amsema Dkt
Mafumiko
Aidha Dkt Mafumiko amewataka kuwa na
utaratibu wa kutoa taarifa kwa wakati pindi wanakumbana na matatizo wakati wa
usafirishaji wa kemikali hizo kwenye maeneo ambazo wanapita.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Chama cha
Wasafirishaji Tanzania COO-TAT Husein Wandwi amesema wamekuwa na changamoto ya baadhi
ya maderva kutokuwa na elimu ya namna ya kujikinga na aina ya kemikali
wanayoisafirisha.
‘Tunaona hii kwetu nii fursa kubwa sana sisi
kama wasafirishaji kwa sababu mwongozo ukija utataka madereva wote waendeshule au
wale wote wanaohusika katika kusafirisha kemikali wawe na elimu’amesema Wandwi.
Naye Albert Swai kutoka kampuni ya CMTL
Logistic wakihusika na usafirishaji wa kemikali amesema serikali imekuwa
ikiwaonyesha ushirikiano kwa kuwaongezea uelewa wa kielimu ili kuhakikisha kuwa
madhara hayatokei.
Hata hivyo serikali imesema itaendelea kuwajengengea uwezo madereva hao wanaosafirisha kemikali ili waweze kukabiliana na madhara yanayosababishwa na kemikali hizo.
Post a Comment