Waziri wa Madini Dkt. Doto
Biteko pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Ibrahimu Uwizeye
wamezindua Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Uwekezaji katika Sekta ya Madini
yanayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
(JNICC) Jijini Dar es Salaam .
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza jambo na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Mhe. Ibrahimu Uwizeye katika Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini
Waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko amezindua magari saba kati ya magari 40 yanayotarajiwa kutolewa na Serikali kama moja ya mikakati ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini
Waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko akiwa katika moja ya gari ikiwani ni moja ya ishara ya uzinduzi wa magari saba kati ya magari 40.
Baadhi ya magari
ambayo yamezindua leo na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko.
....................................
NA MUSSA KHALID
Serikali kupitia wizara ya madini nchini imesema kuwa itaendelea kudhibiti mianya ya utoroshwaji wa madini lengo ni kuiongezea thamani ili kuhakikisha inaleta tija nchini.
Akizungumza Jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea mabanda katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji wa sekta ya madini Nchini yanayotarajia kuanza Februari 22 hadi 23, Waziri mwenye dhamana ya madini Dkt Dotto Biteko amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza mapato kupitia sekta ya madini.
Aidha Waziri Dkt Biteko amesema serikali imekusudia kuondoa urasimu katika sekta hiyo ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje kuwekeza na kuchangia mapato nchini.
Dkt Biteko akizungumzia mikakati iliyowekwa na Wizara ya Madini kwenye udhibiti wa utoroshaji wa madini,amesema kuwa mikakati iliyowekwa ni pamoja na kuongeza maafisa kwenye usimamizi wa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.
Kwa upande wake Waziri wa nishati na madini Nchini Burundi Ibrahim Uwizeye amesema kama nchi watahakikisha wanatumia fursa ya maonesho hayo katika kujifunza ili waweze kuitumia katika nchi yao pamoja na kuongeza uchumi.
Mkutano huo unatarajiwa kuanza rasmi februari 22 hadi 23 huku viongozi kutoka nchi mbalimbali wanatarajia kuhudhuria mkutano huo ambapo kauli mbiu ni mazingira wezeshi kwa maendeleo ya sekta ya madini Nchini.
Kabla ya uzinduzi huo ,Mapema leo Waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko amezindua magari saba kati ya magari 40 yanayotarajiwa kutolewa na Serikali kama moja ya mikakati ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.
Dkt Biteko amewataka watendaji wa Tume ya Madini kuhakikisha magari hayo yanatunzwa na kuendelea kuchapa kazi kwa ubunifu mkubwa ili kuhakikisha lengo la kukusanya shilingi bilioni 650 kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 linafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula sambamba na kuishukuru Wizara ya Madini kwa ununuzi wa magari kwa ajili ya kutumiwa kwenye shughuli za madini amesema kuwa magari yatarahisisha kwa kiasi kikubwa utendaji kazi kwa kufika maeneo yasiyofikika kirahisi.
Post a Comment