JSON WATOA WAONYESHA UPENDO KWA WATOTO WANAOISHI KIJIJI CHA SOS

 Na Mwandiahi Wetu


KAMPUNI ya JSON INVESTMENT LTD) inayojihusisha na urekebishaji wa magari na masuala mazima ya magari ( JSON INVESTMENT LTD) imewatembelea watoto wenye uhitaji wa kijiji cha Children's Village (SOS).


Akizungumza na watoto wakati wa kutoa msaada huo, kituoni hapo Ubungo jijini Dar es Salaam, John Muro amesema kuwa tulichokitoa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii.


"Watoto wanahitaji kuonyeshwa upendo waweze kufarijika kwa kuona wanatembelewa na kupatiwa mahitaji tofauti tofauti kama vifaa vya shule, Michele, unga na vitu vingine vingi."


"Huu ni mwanzo nadhani tutaendelea kutembelea na watoto wengine kwenye uhitaji ili kuwaonyesha upendo na kuwafariji kwa zawadi mbalimbali" amesema Muro


Aidha aliongeza kuwa, tutahakikisha tunashiriki matukio mbalimbali kwenye jamii ili kuleta mahusiano mazuri zaidi na jamii na kurudisha kwa kile tunachokipata.


Kwa upande wake moja ya mlezi wa watoto hao, kijiji cha SOS  Fatuma Stambul, amesema kuwa kila mtoto ana mama yake wa kituo ambaye anamlea, na kumwangalia kwa kila jambo.


"Wapo watoto ambao ni  yatima kabisa hawana wazazi na wengi tunaletewa na Ustawi wa jamii hapa tunawapokea na kuwalea." amesema Fatuma.




0/Post a Comment/Comments